iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.
iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.



Link to original content: https://sw.wikipedia.org/wiki/Waamori
Waamori - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Waamori

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Waamori (kwa Kisumeri 𒈥𒌅 MAR.TU; kwa Kiakadi Tidnum au Amurrūm; kwa Kimisri Amar; kwa Kiebrania אמורי ʼĔmōrī; kwa Kigiriki Ἀμορραῖοι) walikuwa watu wa jamii ya Wasemiti[1][2][3][4] kutoka Syria walioenea pia katika maeneo makubwa ya Mesopotamia kusini kuanzia karne ya 21 KK hadi mwisho wa karne ya 17 KK, wakianzisha idadi kadhaa ya miji-dola muhimu, hasa Babuloni.

Kisha kufukuzwa kutoka Mesopotamia, huko Syria walitawaliwa kwanza na Wahiti, halafu na Waashuru (tangu 1365).

Baada ya 1200 KK hawaonekani tena: inaonekana walimezwa na Wasemiti wengine, ambao kati yao walijitokea hasa Waaramu.

Miji-dola

[hariri | hariri chanzo]

Huko Syria na kandokando:

Huko Mesopotamia:

Katika Biblia

[hariri | hariri chanzo]
Maangamizi ya jeshi la Waamori yalivyochorwa na Gustave Doré.

Katika Biblia Waamori ni wakazi wa milima ya Kaanani, ambao kadiri ya kitabu cha Mwanzo 10:16 wametokana na Kanaan, mwana wa Hamu na mjukuu wa Nuhu. Wanaonekana kama sehemu ya Wakaanani.

Wanatajwa kama watu warefu sana kama "mierezi" (Am 2:9) [5]. Mfalme wao Ogu anatajwa kama jitu la mwisho (Kumb 3:11).

  1. "Amorite (people)". Encyclopædia Britannica online. Encyclopædia Britannica Inc. Iliwekwa mnamo 30 Novemba 2012.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Who Were the Amorites?, by Alfred Haldar, 1971, Brill Archive
  3. Semitic Studies, Volume 1, by Alan Kaye, Otto Harrassowitz Verlag, 1991, p.867
  4. The Semitic Languages, by Stefan Weninger, Walter de Gruyter, 23 Dec 2011, p.361
  5. The height and strength mentioned in Amos 2:9 has led some Christian scholars, including Orville J. Nave, who wrote the classic Nave's Topical Bible, to refer to the Amorites as "giants". http://www.biblestudytools.com/concordances/naves-topical-bible/amorites.html Nave's Topical Bible: Amorites], Nave, Orville J., Retrieved:2013-03-14
  • E. Chiera, Sumerian Epics and Myths, Chicago, 1934, Nos.58 and 112;
  • E. Chiera, Sumerian Texts of Varied Contents, Chicago, 1934, No.3.;
  • H. Frankfort, AAO, pp. 54–8;
  • F.R. Fraus, FWH, I (1954);
  • G. Roux, Ancient Iraq, London, 1980.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Waamori kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.