iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.
iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.



Link to original content: https://sw.wikipedia.org/wiki/Ufilipino
Ufilipino - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Ufilipino

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Repúbliká ng̃ Pilipinas
Jamhuri ya Ufilipino
Bendera ya Ufilipino Nembo ya Ufilipino
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Maka-Diyos, Makatao, Makakalikasan, at Makabansa
("Kwa Mungu, watu, mazingira na nchi")
Wimbo wa taifa: Lupang Hinirang ("Nchi teule")
Lokeshen ya Ufilipino
Mji mkuu Manila
14°35′ N 121°0′ E
Mji mkubwa nchini Quezon City
Lugha rasmi Kitagalog na Kiingereza*
Serikali Jamhuri
Rodrigo Duterte
Leni Robredo
Uhuru
Ilitangazwa
kujitawala
Ilitambuliwa
Katiba

12 Juni 1898
24 Machi 1934
4 Julai 1946
2 Februari 1987
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
300,000 km² (ya 73)
0.64
Idadi ya watu
 - 2015 kadirio
 - 2010 sensa
 - Msongamano wa watu
 
102,291,200 (ya 12)
92,337,852
340.97/km² (ya 43)
Fedha Philippine peso (piso) (PHP)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
PST (UTC+8)
(UTC)
Intaneti TLD .ph
Kodi ya simu +63
* Kicebuano, Kiilokano, Kihiligaynon, Kibikol, Kiwaray-waray, Likapampangan, Kipangasinan, Kinaray-a , Kimaranao , Kimaguindanao, Kitagalog, Kitausug ni lugha rasmi kieneo. Kihispania na Kiarabu hutambuliwa kwa msingi wa matumizi ya hiari.



Ufilipino (kwa Kitagalog: Pilipinas), ni nchi ya kisiwani kwenye Funguvisiwa la Malay katika Asia ya Kusini-Mashariki.

Ina visiwa 7,107 vyenye eneo la km² 300,000.

Mji mkuu ni Manila.

Jiografia ya Ufilipino.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Ufilipino ina visiwa 7,107 vinavyohesabiwa katika makundi matatu yanayoitwa kufuatana na ujirani na visiwa vikubwa vya:

Luzon ni kisiwa kikubwa na Mindanao ni kisiwa cha pili. Visaya ni kundi la visiwa katikati ya funguvisiwa.

Mji mkuu wa Manila uko Luzon. Quezon City ni mji mkubwa. Cebu City ni mji mkubwa upande wa Visaya. Davao City ni mji mkuu wa Mindanao.

Mwaka 1543 nchi iliitwa na Ruy López de Villalobos kwa jina la Kihispania "Las Islas Filipinas" (Visiwa vya Filipo) kwa heshima ya mfalme Filipo II wa Hispania.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Wanegritos ni kati ya wakazi asilia ya funguvisiwa hilo, wakifuatwa na Waaustronesia.

Baadaye kukawa na athira ya Wachina, Wamalay, Wahindi na Wamori.

Hispania ilitawala eneo hilo tangu mwaka 1565 hadi Mapinduzi ya Ufilipino ya 1896, ikiacha athari kubwa upande wa dini na utamaduni.

Marekani ilitwaa visiwa hivyo mwaka 1898 katika Vita ya Marekani dhidi Hispania na kuvitawala kama koloni hadi Vita Kuu ya Pili ya Dunia wakati Japani ilipotwaa nchi kwa miaka minne.

Baada ya vita Ufilipino ikapewa uhuru wake.

Siasa na serikali

[hariri | hariri chanzo]

Ufilipino ina serikali ya urais, tena ya umoja (na tofauti kiasi, sababu baadhi ya maeneo yana uhuru mkubwa kutoka serikali ya kitaifa) ambapo Rais ni mkuu wa nchi na kiongozi wa serikali, pia ni kamanda mkuu wa majeshi. Rais huchaguliwa kwa kura ya umma kwa kipindi kimoja cha miaka sita, wakati ambapo yeye huteua na kusimamia baraza la mawaziri.

Kongamano la bunge limeundwa na Seneti, inayohudumu kama jumba kuu linalo wajumbe waliochaguliwa kwa muda wa miaka sita, na Baraza la Wawakilishi, linalohudumu kama jumba dogo, inayo wajumbe waliochaguliwa kwa muda wa miaka mitatu kutoka kwa wilaya za bunge na kupitia sekta za uwakilishi.

Nguvu za kimahakama zimewekwa katika Mahakama Tukufu iliyoundwa na Jaji Mkuu kama afisa msimamizi, na majaji washirikishi kumi na wanne, wote walioteuliwa na Rais kutoka mapendekezo ya Baraza la Mahakama na Korti.

Kumekuwa na majaribio ya kubadilisha serikali iwe shirikisho, ya bunge kuwa moja au serikali ubunge mwanzo katika muda wa Ramos hadi sasa.

Kuna mikoa ifuatayo:

Wananchi wana asili tofauti sana, kutokana na jiografia na historia ya visiwa hivyo. Mbali na makabila ya wenyeji, kuna Wachina wengi (milioni 2) na machotara wengi sana wenye damu ya Kichina (milioni 18).

Wafilipino milioni 12 wanaishi nje ya nchi.

Wakazi wengi wa Ufilipino hufuata Ukristo wa Kikatoliki (79%) ambao ni urithi wa athira ya Wahispania. Hata hivyo Ufilipino ni nchi isiyo na dini rasmi. Wakristo wengine wanakaribia 10%.

Lugha ya Kiingereza iliachwa na Marekani kama lugha rasmi pamoja na Kifilipino; pia kuna lugha 182 za asili (angalia orodha ya lugha za Ufilipino).

Athira ya Uislamu huonekana hasa kusini mwa kisiwa cha Mindanaoː kwa jumla 5-10% za Wafilipino ni Waislamu wa madhehebu ya Sunni. 2% wanafuata dini za jadi na 1% Ubuddha.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Tovuti rasmi
Biashara
Taarifa za jumla
Vitabu na makala
Wikimedia
Vingine
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ufilipino kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.