Thomas Cranmer
Thomas Cranmer (2 Julai 1489 – 21 Machi 1556) alikuwa Askofu Mkuu wa Canterbury na kiongozi wa Matengenezo ya Kanisa la Uingereza enzi za wafalme Henry VIII, Edward VI na malkia Mary I.
Alisaidia kujenga kesi ya kubatilishwa kwa ndoa ya Henry VIII na Katarina wa Aragon. Talaka hiyo ilikuwa mojawapo ya sababu za kutengana kwa Kanisa la Uingereza na Kanisa Katoliki chini ya Papa wa Roma. Pamoja na Thomas Cromwell aliunga mkono kanuni ya ukuu wa kifalme. Hapo alikubali mamlaka ya mfalme juu ya Kanisa ndani ya milki yake. Aliuawa chini ya malkia Mary alipokataa kurudi katika Ukatoliki.
Mtengenezaji wa Kanisa la Uingereza
[hariri | hariri chanzo]Wakati wa uongozi wake kama Askofu Mkuu wa Canterbury Cranmer alianzisha mabadiliko katika mafundisho na liturgia ya Kanisa la Uingereza. Wakati wa utawala wa mfalme Henry VIII, Cranmer hakufanya mabadiliko mengi.
Alitunga utaratibu wa ibada ya kwanza uliotafsiriwa kwa lugha ya Kiingereza badala ya Kilatini.
Chini ya mfalme Edward VI, aliyemfuata Henry VIII, Cranmer aliweza kuleta mabadiliko mengi zaidi. Alitunga matoleo mawili ya kwanza ya Kitabu cha Sala kwa Watu (Book of Common Prayer) chenye liturgia kamili kwa ajili ya Kanisa la Uingereza. Alipokea wanamatengenezo kadhaa kutoka Ulaya Bara waliofika kama wakimbizi kutoka maeneo chini ya serikali za Kikatoliki. Walimsaidia kubadilisha mafundisho kuhusu mambo kama vile ekaristi, useja wa makasisi, nafasi ya sanamu makanisani na heshima kwa watakatifu. Cranmer alieneza mafundisho mapya, pamoja na Kitabu cha sala, kwa vitabu viwili vya mahubiri (hotuba) yaliyotakiwa kusomwa na mapadre katika ibada makanisani.
Kifo chini ya Malkia Mary
[hariri | hariri chanzo]Baada ya Edward VI, malkia Mary I alichukua madaraka; alikuwa Mkatoliki akalenga kurudisha nchi chini ya Kanisa Katoliki. Aliagiza kumkamata Cranmer na kumshtaki kwa uhaini na uzushi. Alipelekwa mbele ya mahakama ya mahakimu Wakatoliki pamoja na wasaidizi wawili. Wote walihukumiwa adhabu ya kifo cha kuchomwa hai motoni ambayo ilikuwa adhabu ya wazushi.
Katika miaka miwili alipokaa gerezani, Cranmer alipaswa kushuhudia kuchomwa kwa wenzake. Baadaye alijaribu kuokoa uhai wake kwa kukana mafundisho yake ya awali. Kwa kawaida angesamehewa baada ya kukana, lakini malkia Mary I hakutaka kumsamehe bali auawe. Siku ya hukumu yake aliambiwa kusoma tena ukanisho wake kanisani mbele ya watu kabla ya kufa. Cranmer alitumia nafasi hiyo kuonyesha masikitiko juu ya udhaifu wake akamtaja Papa kama mwongo na adui wa Kristo. Hivyo alichomwa akafa kama mzushi kwa Wakatoliki na mfia imani kwa Kanisa Anglikana lililoendelea baadaye kwenye misingi aliyowahi kuweka.
Urithi wake unaendelea katika Kitabu cha Sala kwa Watu Wote na Hoja Thelathini na Tisa ambayo ni ungamo la imani ya Kianglikana linalotokana na kazi yake.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Vyanzo
[hariri | hariri chanzo]- Avis, Paul (2005). "The Revision of the Ordinal in the Church of England 1550–2005". Ecclesiology. 1 (2): 95–110. doi:10.1177/1744136605051929. ISSN 1744-1366.* Ayris, Paul (1993a). "God's Vicegerent and Christ's Vicar: the Relationship between the Crown and the Archbishopric of Canterbury, 1533–53". Katika Ayris, Paul; Selwyn, David (whr.). Thomas Cranmer: Churchman and Scholar. Woodbridge, Suffolk, UK: The Boydell Press. ISBN 0-85115-549-9.
- Ayris, Paul (1993b). "Canon Law Studies". Katika Ayris, Paul; Selwyn, David (whr.). Thomas Cranmer: Churchman and Scholar. Woodbridge, Suffolk, UK: The Boydell Press. ISBN 0-85115-549-9.
- Ayris, Paul (2001). "The Correspondence of Thomas Cranmer, Archbishop of Canterbury, and his English Audience 1533-54". Reformation & Renaissance Review. 3 (1): 9–33. doi:10.1558/rrr.v0i3.9. ISSN 1462-2459. S2CID 170741842.* Ayris, Paul (2002). "The Public Career of Thomas Cranmer". Reformation & Renaissance Review. 4 (1): 75–125. doi:10.1558/rrr.v0i4.75. ISSN 1462-2459. S2CID 145396417.* Bagchi, David V. N.; Steinmetz, David Curtis, whr. (2004). The Cambridge Companion to Reformation Theology. Cambridge: Cambridge University Press. ISBN 0-521-77662-7.
- Bernard, G. W. (2005). The King's Reformation: Henry VIII and the Remaking of the English Church. London: Yale University Press. ISBN 0-300-12271-3.
- Brown, Cornelius (1891). "Ch VIII". A History of Nottinghamshire. E. Stock.
- Coleman-Norton, P. R. (1929). "The Correspondence of S. John Chrysostom (With Special Reference to His Epistles to Pope S. Innocent I)". Classical Philology. 24 (3): 279. doi:10.1086/361140. S2CID 162281389.* Dowling, Maria (1993). "Cranmer as Humanist Reformer". Katika Ayris, Paul; Selwyn, David (whr.). Thomas Cranmer: Churchman and Scholar. Woodbridge, Suffolk, UK: The Boydell Press. ISBN 0-85115-549-9.
- Hall, Basil (1993a). "Cranmer's Relations with Erasmianism and Lutheranism". Katika Ayris, Paul; Selwyn, David (whr.). Thomas Cranmer: Churchman and Scholar. Woodbridge, Suffolk, UK: The Boydell Press. ISBN 0-85115-549-9.
- Hall, Basil (1993b). "Cranmer, the Eucharist, and the Foreign Divines in the Reign of Edward VI". Katika Ayris, Paul; Selwyn, David (whr.). Thomas Cranmer: Churchman and Scholar. Woodbridge, Suffolk, UK: The Boydell Press. ISBN 0-85115-549-9.
- Heinze, Rudolph W. (1993). "'I pray God to grant that I may endure to the end': A New Look at the Martyrdom of Thomas Cranmer". Katika Ayris, Paul; Selwyn, David (whr.). Thomas Cranmer: Churchman and Scholar. Woodbridge, Suffolk, UK: The Boydell Press. ISBN 0-85115-549-9.
- Hirst, Rev E, (Vicar of St. Paul’s Stockport) (1934). "Archbishop Cranmer" (PDF). Churchman Journal. 48 (2): 2. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka (PDF) kutoka chanzo mnamo 7 Novemba 2018. Iliwekwa mnamo 7 Novemba 2018.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: multiple names: authors list (link) - Howell, Thomas Bayly, mhr. (1816). A Complete Collection of State Trials and Proceedings for High Treason and Other Crimes and Misdemeanors from the Earliest Period to the Year 1783. London: T. C. Hansard. OCLC 3815652.
- Loades, David (1993). "Thomas Cranmer and John Dudley: An Uneasy Alliance, 1549–1553". Katika Ayris, Paul; Selwyn, David (whr.). Thomas Cranmer: Churchman and Scholar. Woodbridge, Suffolk, UK: The Boydell Press. ISBN 0-85115-549-9.
- Loades, David M. (2004). Intrigue and Treason: The Tudor Court, 1547–1558. Harlow, England: Pearson Longman. ISBN 0-582-77226-5.
- MacCulloch, Diarmaid (1996). Thomas Cranmer: A Life. London: Yale University Press. ISBN 0-300-06688-0.
- MacCulloch, Diarmaid (2016). All Things Made New: The Reformation and Its Legacy. Oxford University Press. ISBN 978-0-19-061682-3.
- Marshall, Peter (2017). Heretics and Believers: A History of the English Reformation. Yale University Press. ISBN 978-0-300-17062-7.
- Matthew, H. C. G.; Harrison, Brian Howard, eds. (2004). "Oxford Dictionary of National Biography". Oxford Dictionary of National Biography. Oxford: Oxford University Press.
.
- Mills, Jon (2010). "Genocide and Ethnocide: The Suppression of the Cornish Language". Katika Partridge, John (mhr.). Interfaces in Language. Cambridge Scholars Publishing. ISBN 978-1-4438-2433-0.
- Null, Ashley (2006). Thomas Cranmer's Doctrine of Repentance: Renewing the Power to Love. Oxford: Oxford University Press. ISBN 0-19-827021-6.
- Overell, Anne (2008). Italian reform and English Reformations, c.1535-c.1585. Farnham, Surrey, UK: Ashgate Publishing. ISBN 978-0-7546-5579-4.
- Perceval, Arthur Philip (1841). An Apology for the Doctrine of Apostolical Succession: With an Appendix, on the English Orders (tol. la second). London: Rivington.
- Ridley, Jasper (1962). Thomas Cranmer. Oxford: Clarendon Press. OCLC 398369.
- Robinson, Ian (1998). The Establishment of Modern English Prose in the Reformation and the Enlightenment. Cambridge: Cambridge University Press. ISBN 0-521-48088-4.
- Schofield, John (2008). The Rise & Fall of Thomas Cromwell. Stroud, England: The History Press. ISBN 978-0-7524-4604-2.
- Selwyn, D. G. (1993). "Cranmer's Library". Katika Ayris, Paul; Selwyn, David (whr.). Thomas Cranmer: Churchman and Scholar. Woodbridge, Suffolk, UK: The Boydell Press. ISBN 0-85115-549-9.
- Spinks, Bryan D. (1993). "Treasures Old and New: A Look at Some of Thomas Cranmer's Methods of Liturgical Compilation". Katika Ayris, Paul; Selwyn, David (whr.). Thomas Cranmer: Churchman and Scholar. Woodbridge, Suffolk, UK: The Boydell Press. ISBN 0-85115-549-9.
- Stevenson, Kenneth W. (1993). "Cranmer's Marriage Vow: Its Place in the Tradition". Katika Ayris, Paul; Selwyn, David (whr.). Thomas Cranmer: Churchman and Scholar. Woodbridge, Suffolk, UK: The Boydell Press. ISBN 0-85115-549-9.
- Strype, John (1840) [1544]. "Chapter 28". Historical and Biographical Works: Memorials of Thomas Cranmer.