iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.
iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.



Link to original content: https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarumbeta
Tarumbeta - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Tarumbeta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Louis Armstrong akipiga tarumpeta
Tarumbeta

Tarumbeta ni ala ya muziki ya kupuliza ikitengenezwa kwa metali hasa shaba nyeupe. Upande wa mdomo ni nyembamba na upande wa mwisho ni pana yenye. Urefu wa bomba lake linaweza kukaribia mita 1 na nusu lakini bomba hili limepindwa mara mbili kwa kuwa na ala isiyo ndefu mno. Katikati huwa na vilango 3 vinavyobadilisha njia ya hewa na kusababisha sauti kuwa juu na chini.

Sauti yenyewe haufanywi na tarumpeta -tofauti na filimbi- lakini kwa kupuliza hewa baina ya midomo iliyokazwa ndani ya mdomo wa tarumpeta. Ala inapazia sauti hii na kuibadilisha.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Ala kama tarumpeta zimepatikana tangu miaka mielfu lakini zilifanana na ala metalia za kupuliza nyingine hadi mnamo 1830 tarumpeta yenye milango ilitengenezwa.

Ni ala inayopendwa katika Muziki wa Klasiki lakini pia katika muziki wa jadi katika sehemu mbalimbali za dunia. Imekuwa maarufu kama ala ya muziki wa Jazz.

Wapiga tarumbeta

[hariri | hariri chanzo]

Kati wapiga tarumpeta wa muzikiw a klasiki ni Adolph Herseth, Sergei Nakariakov na Maurice Andre.

Katika fani ya jazz ni kwa mfano Miles Davis, Louis Armstrong, Arturo Sandoval, Wynton Marsalis, Dizzy Gillepsie, na Maynard Ferguson waliokuwa maarufu kutokana na ustadi wao wa tarumpeta.