Silika (kemia)
Mandhari
Kuhusu tabia za watu angalia hapa: Silika
Silika au dioksidi ya silikoni (ing: silica, silicon dioxide) ni kampaundi ya kikemia ya oksijeni na silikoni. Alama yake ni SiO2.
Silika inafanya sehemu kubwa ya mchanga unaopatikana duniani. Silika safi huyeyushwa na kutumiwa kwa kutengeneza kioo. Pamoja na saruji hukorogwa kuwa zege.
Silika hutokea kiasili kwa umbo la miamba mbalimbali, hasa shondo (quartz). Inapatikana kwa wingi maana ni sehemu kubwa ya ganda la Dunia.