iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.
iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.



Link to original content: https://sw.wikipedia.org/wiki/Okjeo
Okjeo - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Okjeo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Okjeo

Okjeo ilikuwa nchi ya kabira dogo ambalo liliibukia huko mjini kaskazini mwa Peninsula ya Korea huenda ikawa kuanzia karne ya 2 KK mpaka karne ya 5 CE.

Dong-okjeo (Okjeo Mashariki) kwa haraka-haraka ilichukua eneo la mikoa ya Hamgyŏng ya Korea Kaskazini, na Buk-okjeo (Okjeo Kaskazini) ikachukua kanda ya Mto Duman. Dong-okjeo ilikuwa ikiitwa kwa kifupi kama Okjeo, wakati Buk-okjeo nayo pia ilikuwa ikiitwa kama Chiguru (置溝婁, 치구루) au Guru (구루), mwishoni jina pia lilitumiwa kama Goguryeo. Okjeo imepakana na kijinchi kadogo ka Dongye kwa upande wa kusini, na kushirikiana hatma moja.

Historia

[hariri | hariri chanzo]
Proto-Three Kingdoms, c. 001 AD.

Katika historia yake ya awali, Okjeo ilitawaliwa kati ya utawala wa Kichina na ule wa Goguryeo pia. [1] Kuanzia karne ya tatu KK hadi 108 KK, ilikuwa ikitawaliwa na Gojoseon. [2] Kwa kufuatia kungiliana mara kwa mara na majirani zake, Okjeo haikuweza kukua vyema na kudhibiti ufalme wake.

Wakati wa karne ya 1 au ya 2 CE, Mfalme Taejo wa Goguryeo amepunguza mifereji inayoelekea Okjeo, ambayo ilikuwa ikipitishia bidhaa mitaani mwa Goguryeo. Wakati wa Uvamizi wa Kivita wa Wei wa Goguryeo mnamo 244, Mfalme wa Goguryeo Dongcheon akarudisha majeshi ya kiviti upande wa Kaskazini mwa Okjeo, na mnamo 285, makazi ya kifalme ya Buyeo yakakimbilia huko Okjeo baada ya mashambulizi yaliyokuwa kifanywa mara kwa mara na wahamiaji wa kiskazini.

Mwanzoni mwa karne ya 5, Okjeo ikawa imechukuliwa kabisa na Mfalme Gwanggaeto Taewang wa Goguryeo.

Lugha na utamaduni

[hariri | hariri chanzo]

Ufahamu wetu wa utamaduni wa Okjeo ulikuwa mdogo sana. Kama jinsi ilivyo Dongye, lugha ya Okjeo, chakula, mavazi, ujenzi, na mira zilikuwa sawa tu na za Goguryeo. Watu wa Okjeo wanatekeleza mipango ya harusi ya mtoto kuoa akiwa mdogo na kuishi katika familia hadi ukubwani mwake, wanaizika miili ya familia iliokufa kwenye jeneza moja.

  1. Byeon 1999, p. 49.
  2. Utawala wa Gojoseon ndani ya Okjeo

Byeon Tae-seop (변태섭) (1999). 韓國史通論 (Hanguksa tongnon) (Outline of Korean history), 4th ed. ISBN 89-445-9101-6.

Lee, K. (1984). A new history of korea. Tr. by E.W. Wagner & E.J. Schulz, based on the 1979 Korean ed. Seoul: Iljogak. ISBN 89-337-0204-0

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]