Nzi mweleaji
Nzi mweleaji | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Bango la nzi weleaji (spishi za picha 5 na 7 tu zinatokea Afrika ya Mashariki
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Nusufamilia 4:
|
Nzi weleaji (kutoka kwa Kiing. hoverflies) ni nzi wa familia Syrphidae katika oda Diptera wanaojulikana kwa tabia yao ya kuelea angani. Spishi nyingi huiga nyigu au nyuki kwa rangi zao mara nyingi kali sana. Nzi-nyuki huelea pia, lakini hawa wana nywele nyingi kwa kawaida.
Maelezo
[hariri | hariri chanzo]Urefu wa nzi weleaji huanzia mm 3 hadi 21[1][2]. Umbo lao hutofautiana kutoka kwa mrefu na mwembamba hadi mkubwa na mwenye nywele nyingi. Spishi nyingi zina madoa na/au milia ya rangi kali kama njano, nyekundu au kahawianyekundu. Hata hivyo, wengine ni takriban kabisa nyeusi, kahawia au hata kijani[3]. Baadhi ya rangi husababishwa na akisiko la mwanga na kubadilika kulingana na pembe ya mwanga. Spishi zenye rangi kali hufanana na nyigu au nyuki na hujaribu kuwadanganya mbuai kwa njia hiyo. Hii inaitwa uigizo (mimicry).
Isipokuwa wachache[4], nzi weleaji wanatofautishwa na inzi wengine kwa kuwa na vena bandia ulio sambamba na vena yao ya nne ya kingoringori ya mabawa[1]. Porini, hii ni ngumu kuonwa na huko wanatambuliwa kwa urahisi zaidi na tabia yao ya kuelea. Hata hivyo, hawaelei wakati wa kujilisha. Hiyo ni njia rahisi ya kuwatofautisha na nzi-nyuki, ambao kwa kweli huelea wakati wa kujilisha, isipokuwa kwa idadi ndogo ya spishi, na pia huiga nyuki. Kwa njia nyinginezo za kutofautisha makundi haya mawili ya nzi, angalia makala kuhusu nzi-nyuki.
Wapevu hujilisha kwa mbochi na chavua[3]. Mabuu, kwa upande mwingine, hula vyakula mbalimbali. Baadhi hujilisha kwa dutu ya mimea au wanyama zinazooza, huku wengine hula vidukari, tiripsi na wadudu wengine wanaonyonya mimea[1][5]. Spishi mbuai hufaidia wakulima na watunza bustani, kwani vidukari huharibu mazao, na mabuu wa nzi weleaji hutumiwa mara nyingi katika udhibiti wa kibiolojia. Hii ni pamoja na mojawapo ya spishi zinazoenea sana za nzi weleaji, Episyrphus balteatus, ambaye mabuu yake hula vidukari. Spishi fulani, kama vile Merodon equestris au Eumerus tuberculatus, zinawajibika kwa uchavushaji.
Mabuu ya spishi fulani huishi majini, kama vile mabuu ya Eristalis tenax. Wana neli ya kupumulia kwenye ncha yao ya nyuma na kwa sababu ya hiyo huitwa mabuu wenye mkia wa panya[1]. Huishi katika maji yaliyotuama, hata maji taka[6]. Mara kwa mara wanaweza kuendelea kuishi ndani ya matumbo baada ya kumezwa kwa bahati mbaya na kusababisha shida kidogo kabla ya kutolewa nje[7].
Spishi kadhaa za Afrika ya Mashriki
[hariri | hariri chanzo]
|
|
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Eristalinus aeneus
-
Eristalinus megacephalus
-
Eristalis tenax
-
Eumerus feae
-
Eumerus paulae
-
Eupeodes corollae
-
Melanostoma scalare
-
Ornidia obesa
-
Paragus haemorrhous
-
Sphaerophoria rueppelli
- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 "Hover fly". Encyclopædia Britannica Online. 2009. https://www.britannica.com/EBchecked/topic/273341/hover-fly. Retrieved December 5, 2009.
- ↑ Stubbs, Alan E.; Falk, Steven J (1983). British Hoverflies: An Illustrated Identification Guide (tol. la 2nd). London: British Entomological and Natural History Society. ku. 253, xvpp. ISBN 1-899935-03-7.
- ↑ 3.0 3.1 "Hoverfly". Hutchinson Encyclopedia. Helicon Publishing. 2009. http://encyclopedia.farlex.com/Hover+Fly. Retrieved December 6, 2009. Archived 8 Machi 2012 at the Wayback Machine. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-03-08. Iliwekwa mnamo 2022-09-30.
- ↑ Reemer, Menno (2008). "Surimyia, a new genus of Microdontinae, with notes on Paragodon Thompson, 1969 (Diptera, Syrphidae)" (PDF). Zoologische Mededelingen. 82: 177–188.
- ↑ Schmidt, Martin; Thewes, Ulrich; Thies, Carsten; Tscharntke, Teja (2004). "Aphid suppression in mulched cereals". Entomologia Experimentalis et Applicata. 113 (2): 87–93. doi:10.1111/j.0013-8703.2004.00205.x. S2CID 85070615.
- ↑ Aguilera A, Cid A, Regueiro BJ, Prieto JM, Noya M (Septemba 1999). "Intestinal myiasis caused by Eristalis tenax". Journal of Clinical Microbiology. 37 (9): 3082. doi:10.1128/JCM.37.9.3082-3082.1999. PMC 85471. PMID 10475752.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Whish-Wilson PB (2000). "A possible case of intestinal myiasis due to Eristalis tenax". The Medical Journal of Australia. 173 (11–12): 652. doi:10.5694/j.1326-5377.2000.tb139374.x. PMID 11379520. S2CID 12898612.