Miporomoko ya ardhi
Miporomoko ya ardhi (kwa Kiingereza landslide) hutokea pale ambako miamba, mchanga, au vifusi vinaposonga chini kwenye mteremko. Mitiririko ya vifusi, ambayo pia huitwa mimonyoko ya udongo, ni aina ya mporomoko wa ardhi inayotokea kwa kasi sana yenye mwelekeo wa mfereji.
Kisababishi cha miporomoko ya ardhi na mitiririko ya vifusi
[hariri | hariri chanzo]Miporomoko ya ardhi husababishwa na vurugu katika uthabiti asilia wa mteremko. Zinaweza kuandamana na mvua kubwa au kufuata ukame, mitetemeko ya ardhi au kufoka kwa volkano. Mimomonyoko ya udongo hutokea maji yanapokusanyika kwa haraka ardhini na kusababisha kufura kwa mwamba, ardhi, na vifusi vilivyojaa maji. Mimonyoko ya udongo huanza kwa miteremko mikali na inaweza kuchochewa na maafa ya asilia. Maeneo ambayo mioto inayoenea kwa kasi au ubadilishaji wa ardhi na binadamu imeharibu mimea katika miteremko yana uwezekano mkubwa hasa wa miporomoko ya ardhi wakati wa na baada ya mvua kubwa.
Tishio za kiafya kutokana na miporomoko ya ardhi na mitiririko ya vifusi
[hariri | hariri chanzo]Hatari za kiafya zinazohusishwa na miporomoko ya ardhi na mimonyoko ya udongo ni:
- Maji yanayosonga kwa kasi na vifusi vinavyoweza kusababisha kiwewe;
- Nyaya za stima zilizovunjika, maji, gesi, na laini ya maji taka zinazoweza kusababisha jeraha au maradhi; na
- Barabara na mifumo ya reli iliyokatizwa inayoweza kuhatarisha magari na kukatiza usafiri na kufikia huduma ya afya.
Sehemu zilizo hatarini
[hariri | hariri chanzo]Sehemu zingine zina uwezekano mkubwa wa kupatata miporomoko ya ardhi au mimonyoko ya udongo, ikijumuisha:
- Sehemu ambazo moto wa kuenea haraka au ubadilishaji wa ardhi na binadamu imeharibu mimea;
- Sehemu ambazo miporomoko ya ardhi imetokea hapo awali;
- Miteremko mikali na sehemu zilizoko upande wa chini wa mteremko au genge kuu;
- Miteremko iliyobadilishwa kwa ujenzi wa majengo na barabara;
- Milangobahari iliyoko kando ya kijito au mto; na
- Sehemu ambazo njia kavu zimeelekezwa.
Namna ya kujikinga
[hariri | hariri chanzo]Kabla ya dhoruba na mvua kubwa
[hariri | hariri chanzo]- Chukulia kuwa miteremko mikali na maeneo yaliyochomwa na mioto inayoenea kwa kasi ina uwezekano wa miporomoko ya ardhi na mitiririko ya vifusi.
- Fahamu iwapo miporomoko ya ardhi au mitiririko ya vifusi imetokea awali katika eneo lako kwa kuwasiliana na mamlaka ya eneo hilo, mtaalamu wa jiolojia wa kaunti au idara ya mipango ya kaunti, wataalamu wa kupima ramani wa kijiolojia katika nchi, au idara za jiolojia za chuo kikuu.
- Wasiliana na mamlaka ya eneo hilo kuhusu mipango ya dharura na uhamisho.
- Tengeneza mipango ya dharura na ya uhamisho ya familia na biashara yako.
- Tengeneza mpango wa mawasiliano ya dharura iwapo wanajamii wametenganishwa.
- Iwapo unaishi katika eneo lenye uwezekano wa miporomoko ya ardhi fikiria kutoka hapo.
Wakati wa dhoruba na mvua kubwa
[hariri | hariri chanzo]- Sikiliza redio au utazame televisheni kwa maonyo kuhusu mvua kubwa au kwa habari na maagizo kutoka kwa wenye madaraka rasmi wa eneo hilo.
- Fahamu ongezeko au kupungua ghafla kwa viwango vya maji katika mto au hori inayoweza kuashiria mtirirko wa vifusi upande wa juu wa mto. Mchururu wa udongo unaoteremka unaweza kutanguliza mtiririko mkubwa.
- Tafuta miti iliolala upande, nguzo za simu, nyua, au kuta, na kwa mashimo mapya au sehemu wazi katika pande za milima.
- Sikiliza sauti za mngurumo zinazoweza kuashiria mporomoko wa ardhi ao mmonyoko wa udongo unaokaribia.
- Tahadhari unapoendesha gari. Barabara zinaweza kuwa na kizuizi au kufungwa kwa sababu ya njia ya miguu iliyoporomoka au vifusi.
- Iwapo hatari ya mporomoko wa ardhi au mtiririko wa vifusi iko karibu, toka kwa njia ya mporomoko haraka. Kutoka kwa njia ya mtiririko wa vifusi ndio kinga yako bora zaidi. Enda katika eneo lililo juu na karibu sana katika upande mbali na njia hiyo. Iwapo mawe na vifusi inakaribia, kimbia kuelekea mahali pa kujisetiri palipo karibu na ujikinge(Ikiwezekana, chini ya dawati, meza, au samani zingine zozote zenye nguvu.)
Baada ya mporomoko wa ardhi au mtiririko wa vifusi
[hariri | hariri chanzo]- Kaa mbali na eneo hilo. Kufurika au miporomoko zaidi inaweza kutokea baada ya mporomoko wa ardhi au mmonyoko wa udongo.
- Angalia watu waliojeruhiwa au kutegwa karibu na sehemu lililoathirika, ikiwezekana fanya hivyo bila kuingia njia ya mporomoko wa ardhi au mmomonyoko wa udongo.
- Sikiliza redio au televisheni kwa habari ya dharura.
- Piga ripoti kuhusu nyaya zinazotumika zilizovunjika kwa mamlaka husika.
- Tafuta maoni ya mtaalamu wa masuala ya ardhi (mtaalum aliyesajiliwa mwenye umahiri wa uhandisi wa mchanga) kwa ushauri kuhusu kupunguza matatizo nyongeza na hatari ya mporomoko wa ardhi. Mamlaka ya eneo inapaswa iweze kukueleza jinsi ya kuwasiliana na mtaalamu wa masuala ya ardhi.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Banguko (poromoko la theluji na barafu)