iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.
iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.



Link to original content: https://sw.wikipedia.org/wiki/Lewis_Hamilton
Lewis Hamilton - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Lewis Hamilton

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lewis Hamilton
Lewis Hamilton mwaka 2008 kwenye Mashindano ya Sau Paulo, Brazil
Lewis Hamilto mwaka 2008 kwenye Mashindano ya Sau Paulo, Brazil
Jina la kuzaliwa Lewis Carl Davidson Hamilton
Amezaliwa 7 Januari 1985 (1985-01-07) (umri 39)[1]United Kingdom Uingereza
Kazi yake Dereva wa Mashindano ya Magari

Sir Lewis Carl Davidson Hamilton (alizaliwa 7 Januari 1985) ni dereva wa mashindano ya magari kutoka nchini Uingereza, kwa sasa anashindana katika Mbio za Langalanga akiwa na kampuni ya Mercedes-Benz. Hamilton anashikilia rekodi ya kushinda mataji saba ya dereva bora wa msimu akiwa sawa na Michael Schumacher— na anashikilia rekodi ya dereva alieshinda mbio nyingi zaidi za Grand prix (105), nafasi tatu za juu (104) na nafasi kumi za juu (201).

Akiwa amezaliwa na kukulia Stevenage, Hertfordshire, Hamilton alijiunga na program ya madereva wadogo iliyotolewa na McLaren mwaka 1998. Hii ilipelekea kuwa dereva wa McLaren katika Mbio za Langalanga kuanzia mwaka 2007 hadi 2012, hii ilimfaka kuwa mtu wa kwanza mweusi kushiriki kama dereva katika mfululizo wa mashindano hayo. Katika msimu wake wa kwanza, Hamilton aliweka rekodi nyingi, alimaliza nafasi ya pili nyuma ya Kimi Räikkönen kwa tofauti ya alama moja. Katika mashindano ya mwaka 2008, alishinda taji lake la kwanza kwa namna ya kipekee, kwenye Grand prix ya Brazil, alifanikiwa kumpita dereva alikua anaongoza mbio hizo hatua ya mwisho kabisa, ushindi huu ulimfanya kuwa dereva mdogo kuliko wote kuwahi kushinda taji la Mbio za Langalanga kwa wakati ule. Baada ya msimu sita akiwa na McLaren, Hamilton alisign mkataba na kujiungana Mercedes mwaka 2013.

Mabadiliko ya sheria za engine ya magari yam waka 2014, yalikua ndo mwanzo wa mafanikio ya Hamilton, kipindi hicho alishinda mataji sita zaidi. Alishinda mataji mfulilozo mwaka 2014 na 2015, msimu ulikua na ushindani mkali kutoka kwa dereva mwenza Nico Rosberg. Kufuatia kustaafu kwa Rosberg mwaka 2016, Dereva wa kampuni ya Ferrari Sebastian Vettel akawa mshindani mkuu wa Hamilton kwa misimu miwili, ambapo Hamilton aliweza kushinda mataji mfululizo tena, mwaka 2017 na 2018. Taji lake la tat una la nne alipata mwaka 2019 na 2020 na kufanikiwa kufikia rekodi ya Schumacher ya mataji saba kwa dereva. Hamilton alivunja rekodi ya kushinda Grand prix 100 mwaka 2021. Ataondoka Mercedes na kujiunga na Ferrari kuanzia msimu wa 2025 na kuendelea,.

Hamilton anapewa sifa nyingi kwa kuendeleza lengo la Mbio za Langalanga kufuatia mashabiki wengi nje ya mchezo huo, kwa sehemu ikisababishwa na aina ya Maisha yake, pamoja na kuwa mkereketwa wa masuala ya mazingira na jamii na kufuatilia sana masuala ya muziki na fasheni. Amekua pia balozi wa kupinga ubaguzi wa rangi akiwa na lengo ya kusukuma ongezeko la watu wa rangi tofauti katika mashindano ya magari. Hamilton alitajwa katika orodha ya watu 100 wenye ushawishi mkubwa duniani kwenye jarida la 2020 la Time na alipewa heshima ya Knight mwaka 2021.

Maisha ya Utoto na Elimu

[hariri | hariri chanzo]
Hamilton akisherehekea pamoja na baba yake, wakati huo akiwa meneja wake Anthony Hamilton baada ya Grand Prix ya Brazil mwaka 2008[2]

Lewis Carl Davidson Hamilton alizaliwa 7 Januari 1 1985 huko Stevenage, Hertfordshire.[1] Baba yake, Anthony Hamilton, ana asili ya Grenada, na mama yake Carmen Larbalestier, anatokea Uingereza, mji wa Birmingham,[3] hii humfanya kuwa chotara[4] Wazazi wa Hamilton walitengenga akiwa na miaka miwili, aliishi na mama yake pamoja na dada zake wakambo wawili Samantha na Nicola, mpaka alipofikisha miaka kumi na miwili.[5] Baadaye Hamilton aliishi na baba yake, mama yake wa kambo, na kaka yake wa kambo Nicolas ambaye naye ni dereva wa mashindano ya magari.[6][7] Hamilton alilelewa kwenye dhehebu ya Kikatoliki.[8]

Akiwa na umri wa miaka mitano, baba yake alimnunulia gari la kuchezea linaloendeshwa kwa rimoti.[9] Mwaka uliofuatia, Hamilton alimaliza nafasi ya pili kwenye mashindano ya BRCA, mshindani wake akiwa ni mtu mzima.[10] Kwa kuwa Hamilton alikua ndio mtoto pekee mweusi kwenye klabu yao, alikutana na changamoto nyingi za ubaguzi wa rangi.[9][11] Akiwa na umri wa miaka sita, baba yake alimnunulia gari dogo maarufu kwa jina la go-kart, hii ilikua zawadi ya sikukuu ya Noeli, alimuahidi kumuunga mkono kwenye kazi yake ya mashindano ya magari, hii ni endapo angefanya vizuri shuleni.[12] Kama sehemu ya kumsaidia mtoto wake, Baba yake Hamilto aliacha kazi aliyokua anafanya kama Meneja wa kitengo cha Technolojia ya Habari na akaamua kuwa muunda magari, Hii ilimfanya mara nyingi kufanya kazi zaidi ya nne zikiwa ni pamoja na mtu wa mauzo, muosha viombo, na kazi ya kubandika mabango ya madalali,[13] wakati huo wote aliendelea kuhudhuria mashindano ya magari aliyoshiriki mwanae.[14] Baadaye, Baba yake Hamilto alifungua kampuni yake mwenyewe ya Teknolojia ya Mawasiliano.[15] Aliendea kuwa meneja wa Hamilton mpaka mwanzoni mwa mwaka 2010.[16][17]

Hamilton alisoma katika shule ya Saint John Henry Newman, hii ni shule ya Kikatoliki inayopatikana Stevenage.[18] Kutokana na uonevu aliokua akipata shuleni, Hamilton mwenyewe anakiri kwamba aliamua kujifunza mchezo wa karate, lengo likiwa ni kwa ajili ya kujilinda mwenyewe.[19] Kuna kipindi alizuiwa kwenda shule baada ya ksuingiziwa kumshambulia mwanafunzi mwenzake ambaye alipata majeruhi yaliyolazimu kupelekwa hospitali kwa matibabu.[20] Pamoja na kushiriki mashindano ya magari, Hamilton alicheza mpira wa miguu pia, alikua miongoni mwa wachezaje wa timu ya shule, huko alicheza pamoja na Ashley Young.[15] Akiwa ni mshabiki wa klabu ya Arsenal, Hamilton anakiri kwamba endapo asingejihusisha na mashindano ya magari, basi angekua mchezaji wa mpira wa miguu ama mchezo wa Kriketi, hii ni kwasababu alicheza michezo yote kwenye timu za shule.[21] Mnamo Februari 2001, alianza masomo kwenye chou cha Cambridge Arts and Sciences (CATS), iliopo Cambridge.[22]

  1. 1.0 1.1 Kelso, Paul. "Profile: Lewis Hamilton", The Guardian, 20 April 2007. 
  2. Cary, Tom. "Anthony Hamilton's massive support makes parting with Lewis easier to understand", The Daily Telegraph, 3 March 2010. Kigezo:Cbignore
  3. "FreeBMD Entry Info". freebmd.org.uk. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Desemba 2021. Iliwekwa mnamo 12 Desemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Being F1's first black driver is important". lewishamilton.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Machi 2018. Iliwekwa mnamo 7 Machi 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Mathé, Charlotte (12 Julai 2014). "10 Things About ... Lewis Hamilton". Digital Spy. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 20 Agosti 2020. Iliwekwa mnamo 21 Novemba 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. Kigezo:Cite AV media
  7. Matt Dickinson. "Lewis Hamilton admits: 'I just don't know how I kept my cool'", The Times, 3 November 2008. Retrieved on 2024-10-01. Archived from the original on 2009-05-09. 
  8. "Lewis Hamilton Biography – Trivia", The Biography Channel, London: thebiographychannel.co.uk. Retrieved on 2024-10-01. Archived from the original on 2014-05-25. 
  9. 9.0 9.1 "BBC Radio 4 - Radio 4 in Four - Race to the top: Lewis Hamilton". bbc.co.uk. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Oktoba 2020. Iliwekwa mnamo 26 Oktoba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. "Lewis Hamilton Biography". F1Fanatic.co.uk. 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Machi 2009. Iliwekwa mnamo 6 Oktoba 2007.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. "Lewis Hamilton: I had a lot of bullying and racism at school". Eurosport (kwa Kiingereza). 25 Septemba 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Juni 2023. Iliwekwa mnamo 26 Oktoba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  12. Kigezo:Cite magazine
  13. Benson, Andrew. "Challenger, champion, change-maker: The real Lewis Hamilton story". bbc.co.uk. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Novemba 2020. Iliwekwa mnamo 16 Novemba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  14. Classen, Robin (22 Mei 2018). "'Thanks dad!' Lewis Hamilton reflects on his F1 championship journey". Wheels. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 14 Februari 2019. Iliwekwa mnamo 26 Oktoba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  15. 15.0 15.1 Owen, Oliver. "The real deal", The Guardian, 3 June 2007. 
  16. Callow, James. "Lewis Hamilton signs with Simon Fuller's XIX Entertainment", The Guardian, 14 March 2011. 
  17. "Words from Lewis Hamilton's father inspired Hungarian Grand Prix pace, says Wolff | Formula 1®", 5 August 2019. (en) 
  18. "Lewis Hamilton fact file". BBC Southern Counties. BBC. 19 Juni 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 Desemba 2010. Iliwekwa mnamo 31 Agosti 2010.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  19. Davies, Gareth A. "A salute to the real Lewis Hamilton", The Daily Telegraph, 5 July 2007. Kigezo:Cbignore
  20. Younge, Gary (10 Julai 2021). "Lewis Hamilton: 'Everything I'd suppressed came up – I had to speak out'". theguardian.co.uk. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Agosti 2021. Iliwekwa mnamo 10 Julai 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  21. "Lewis Hamilton: I could have been a footballer", The Daily Telegraph, 29 October 2007. 
  22. Hamilton, Lewis (2007). Lewis Hamilton: My Story. HarperCollins. ISBN 978-0-00-727005-7.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lewis Hamilton kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.