iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.
iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.



Link to original content: https://sw.wikipedia.org/wiki/Kondoo-kaya
Kondoo-kaya - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Kondoo-kaya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kwa kundinyota ya Aries inayoitwa pia kondoo, angalia hapa

Kondoo-kaya
Kundi la kondoo
Kundi la kondoo
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Artiodactyla (Wanyama wenye vidole viwili au vinne mguuni)
Nusuoda: Ruminantia (Wanyama wanaocheua)
Familia: Bovidae (Wanyama walio na mnasaba na ng'ombe)
J. E. Gray, 1821
Nusufamilia: Caprinae (Wanyama wanaofanana na mbuzi)
Jenasi: Ovis (Kondoo)
Linnaeus, 1758
Spishi: O. aries (Kondoo-kaya)
Linnaeus, 1758

Kondoo-kaya (Ovis aries) ni mnyama afugwaye na binadamu kwa sababu ya nyama, sufu na pia maziwa. Kondoo hula manyasi na kutembea kwa vidole viwili.

Asili yake ni aina za kondoo wa pori waliofugwa kwa sababu ya nyama na maziwa. Katika nchi yenye baridi sufu au nywele zake inatafutwa sana kwa sababu nguo za sufu ni kinga nzuri dhidi ya baridi.

Wataalamu wamegundua kwamba asili ya kondoo-kaya wote ni kondoo wa porini kutoka Kaukazi ambako ufugaji wa mnyama huyu ulianzishwa na kuenea.

Kondoo wako katika familia Bovidae pamoja na spishi za ng'ombe na kama hawa wanacheua chakula chao na huwa na tumbo lenye vyumba vinne. Baada ya kula nyasi mara ya kwanza wanairudisha kutoka chumba cha kwanza cha tumbo na kuitafuna tena. Kwa njia hii wanapata lishe nyingi kutoka nyasi.

Duniani kuna jumla kondoo-kaya bilioni moja na asilimia 40 wako Asia (China, Uhindi, Uajemi). Afrika Kusini na nchi za Afrika ya Kaskazini (hasa Sudan) wanaishi takriban asilimia 20, Australia na New Zealand tena asilimia 15. Robo inayobaki wako Ulaya (Uingereza) na Amerika.

Kiuchumi matumizi yake siku hizi ni hasa kwa nyama. Maziwa hutumiwa zaidi kwa jibini kama feta. Umuhimu wa sufu umepungua kutokana na uenezaji wa nguo za sintetiki.

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kondoo-kaya kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.