iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.
iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.



Link to original content: https://sw.wikipedia.org/wiki/Kaswende
Kaswende - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Kaswende

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kaswende - Syphilis
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuInfectious diseases, dermatology Edit this on Wikidata
ICD-10A50.-A53.
ICD-9090-097
DiseasesDB29054
MedlinePlus000861
eMedicinemed/2224 emerg/563 derm/413
MeSHD013587
Vipele vya awali vya kaswende katika uume.
Hatua ya pili ya kaswende inavyojitokeza mikononi.
Mfano wa kichwa cha mtu mwenye kaswende katika hatua ya tatu.

Kaswende (ing. syphilis) ni mojawapo kati ya maradhi ya zinaa ambayo inasababishwa na bakteria inayofahamika kama Treponema pallidum.

Katika hatua za mwanzo, vipele katika sehemu za uzazi huanza kujitokeza muda mfupi baada ya maambukizi ambavyo baadaye hupotea vyenyewe.

Kama ugonjwa hautatibiwa, maambukizi huendelea kwa miaka, yakishambulia mifupa, ubongo na moyo na kusababisha madhara mengine yanayotokana na matatizo katika mfumo wa fahamu kama vile homa ya uti wa mgongo na magonjwa ya moyo na kiharusi.

Kaswende wakati wa ujauzito unaweza kuwa hatari kubwa kwa kiumbe tumboni, kama vile kusababisha kutoumbika vizuri (deformity) na kifo.

Wanawake wengi wajawazito katika nchi zilizoendelea huchunguzwa kwa uwepo wa ugonjwa huu katika majuma ya kwanza ya mimba ili kutibu ugonjwa kabla kitoto hakijaathirika.

Siku hizi kaswende inaweza kutibika kwa urahisi fulani kwa penicillin.

Maelezo zaidi ya msingi

Kaswende inasababishwa na bakteria ya spirochete Treponema pallidum baadhi ya spishi pallidum. Njia ya kawaida zaidi ya kuambukizwa ni kupitia ngono; hata hivyo, kaswende pia inaweza kuambukizwa kutoka kwa mama hadi kwa mimba wakati wa ujauzito au wakati wa kuzaliwa kwa mtoto, na kusababisha kuzaliwa na kaswende. Magonjwa mengine ya binadamu yanayohusiana niTreponema pallidumbakteria inajumusiha buba (baadhi ya spishi pertenue), pinta (baadhi ya spishi carateum) na bejel (baadhi ya spishi endemicum).

Dalili na ishara za kaswende hutofautiana kulingana na hatua iliyoko kati ya hatua nne. Hatua ni ya kwanza, ya pili, fiche, na ya mwisho. Hatua ya kwanza kawaida inajitokeza kimoja na shanka utokeaji wa kidonda kwa ngozi isiyowasha, ngumu, isiyokuwa na uchungu). Hatua ya pili ya kaswende hujitokeza na upele ambayo mara kwa mara inahusisha viganja vya mikono na nyayo za miguu. Hatua fiche ya kaswende hujitokeza na dalili kiasi au hata bila. Hatua ya mwisho ya kaswende hujitokeza na guma, dalili zinazohusiana na mfumo wa neva, au zinazohusiana na moyo.

Hata hivyo, kaswende imeitwa "mwiigaji mkuu" sababu mara nyingi hujitokeza kwa njia isiyo ya kawaida.

Kwa kawaida kaswende hutambulika kwa uchunguzi wa damu;hata hivyo, bakteria inaweza kuonekana kwa kutumia hadubini. Kaswende inaweza kutibiwa kwa njia inayofaa kwa kutumia antibiotiki, haswa ndani ya misuli penisilini G. Hii inapendekezwa kwa watu walio na aleji ya penisilini, seftriaksoni.

Inaaminika kwamba kufikia mwaka wa 1999 watu milioni 12 walikuwa wameambukizwa kaswende ulimwenguni na zaidi ya asilimia 90 ya hali hizi kutoka kwa nchi zinazoendelea. Hali za kaswende zilipungua kwa kasi baada ya penisilini kupatikana kwa urahisi katika miaka ya 1940, lakini viwango vya maambukizi vimeongezeka tangu mwaka 2000 katika nchi nyingi. Mara nyingi kaswende hupatikana pamoja na virusi vinavyosababisha UKIMWI (VVU). Hii imehusishwa na sehemu ya matendo ya ngono yasiyokuwa salama kati ya wanaume wanaofanya ngono na wanaume wengine;Ongezeka la uasherati; ukahaba; na kupungua kwa matumizi ya kondomu.[1][2][3]

Dalili na ishara

Kaswende inaweza kuwa katika hatua moja kati ya hatua nne tofauti: ya kwanza, ya pili, fiche, na ya mwisho,[4] na pia inaweza kujitokeza wakati wa kuzaliwa.[5] ilirejelewa kama "mwiigaji mkuu" na Sir William Osler kutokana na njia mbalimbali inavyojitokeza[4][6]

Hatua ya kwanza

Vipele vya awali vya kaswende katika mkono.

Hatua ya kwanza ya kaswende kawaida hupatikana kwa kuwasiliana kwa njia ya moja kwa moja kwa ngono na vidonda vilivyoambukizwa vya mtu mwingine.[7]Takriban siku 3 hadi 90 baada ya kuathiriwa hapo awali ( wastani ya siku 21 ) kidonda kwa ngozi, iitwayo shanka, hutokea mahali palipogusana.[4] Huu ni mfano hasa (Asilimia 40 ya wakati) kidonda kimoja, kigumu, kisichokuwa na uchungu, kisichowasha na sehemu yake ya chini iliyokuwa safi na mipaka mikali kati ya sentimita 0.3 na 3.0 kwa ukubwa .[4] Hata hivyo, kidonda, kinaweza kuonekana kuwa tofauti sana. [8] Katika viwango, hugeuka kutokamacule hadi kipelena kisha kwa uyeyukaji au donda.[8] Mara chache, kutakuwa na vidonda kadhaa. (~40%),[4] Hii pia ni ya kawaida mtu anapoambukizwa Virusi Vya Ukimwi

Shanka yanaweza kuwa na uchungu au nyororo (30%), na zinaweza kutokea nje viungo vya uzazi (2–7%). Mahali pa kawaida zaidi pa chanikeri kwa wanawake ni kwa seviksi(44%). Mahali pa kawaida zaidi kwa wanaume wanaovutiwa na jinsia tofauti ni Kwa uume (99%). Wakati mwingine shanka hutokea kwa tupu ya nyama au rektamu kwawanaume wanaojishirikisha ngono na wanaume wengine (34%).[8] Tenzi kuvimba mara kwa mara (80%)hutokea pahali palipo ambukizwa,[4] hutokea siku 7 hadi 10 baada ya kutokea kwa shanka[8] kidonda kinaweza kuendelea kutokea wiki watatu hadi sita bila matibabu[4]

Hatua ya pili

Nyekundu vipele na vipele kuzidi mwilini kutokana na hatua ya pili ya kaswende

Hatua ya pili ya kaswende hutokea takriban wiki nne hadi kumi baada ya hatua ya kwanza ya maambukizi.[4] hatua ya pili ya ugonjwa unaweza kujitokeza kwa njia nyingi tofauti, lakini kwa kawaida dalili sana sana huhusisha ngozi, membreni ute, na tezi ya limfu.[9] kunaweza kuwa na upele mwekundu-waridi-isiyokuwa na mwasho kwa kiwiliwili pamoja na limbu (miguu na mikono), ikiwa ni pamoja na viganja na nyayo.[4][10] Vipele vinaweza kuwa makulopapula au yenye pustuli. inaweza kutengeneza chunjua kama vidonda iliyopana, nyeupe na sawa sawa inayojulikana kama kondiloma latum kwa membreni yenye utes. Vidonda hivi vyote vinamaambukizi na yanahifadhi bakteria. Dalili zingine inaweza ni pamoja na homa, uchungu wa koo, hitilafu ya mwili,kupunguza uzito, kutokwa na nywele, na maumivu ya kichwa.[4] matokeo yasiyo kuwa ya kawaida ni pamoja na hepatitisi, figo ugonjwa, athritisi,periostitisi, neuritsi ya kuona, uveitisi, na keratitisi ya interstitial.[4][11]

Kwa kawaida dalili kali uyeyuka baadaye kati ya wiki tatu hadi sita;[11] hata hivyo, katika hali iliyokaribia 25%, dalili ya hatua ya pili yanaweza kurudi. Watu wengi walio katika hatua ya pili ya kaswende (40–85% ya wanawake, 20–65% ya wanaume) hawatoi ripoti kuwa na shanka ya kiwango kilicho juu cha hatua ya kwanza ya kaswende.[9]

Hatua fiche

Hatua fiche ya kaswende imefafanuliwa kama kuwa na serologic utambuzi wa maambukizi bila dalili ya magonjwa.[7] Imeelezwa zaidi kama ya hapo awali (chini ya mwaka wa 1 mwaka mmoja baada ya hatua ya pili ya kaswende) katika Marekani[11] Uingerezani, masaa hizi huitwa miaka miwili ya hatua fiche ya kaswende ya mapema na iliyochelewa.[8] Dalili ya hatua fiche ya kaswende ya mapema huweza kurudi tena. Hatua fiche ya kaswende iliyochelewa huwa haina dalili za magonjwa (hayana dalili), na hatua fiche ya kaswende iliyochelewa haiambukizwi kwa urahisi kama hatua fiche ya kaswende ya mapema.[11]

Hatua ya mwisho

Hatua ya mwisho ya kaswende inaweza kutokea takriban miaka mitatu hadi 15 baada ya maambukizi ya kwanza, na inaweza kugawanywa kwa aina tatu tofauti: kaswende iliyosababishwa na guma (15%), iliyochelewa kaswende katika mfumo wa neva (6.5%), na kaswende inayoathiri moyo na mishipa ya damu (10%).[4][11] Bila matibabu, theluthi moja ya watu ambao wameambukizwa kaswende hupata hatua ya mwisho ya kaswende.[11] Watu walio na awamu ya mwisho ya kaswende hawawezi kuambukiza wengine.[4]

Kaswende inayosababishwa na gum, pia inayoitwa hafifu kaswende, kwa kawaida hutokea moja kwa miaka 46 baada ya maambukizi ya awali, kwa wastani wa miaka.15  Hatua hii ni sifa ya muundo sugu wa guma, ambayo ni uvimbe nyororo zinazofanana na vidonge vya inflamesheni vinavyoweza kuwa zinabadilika kulingana na ukubwa. Kawaida huathiri ngozi, mifupa, na ini, lakini inaweza kutokea mahali popote.[4]

Kaswende katika mfumo wa neva inamaanisha maambukizi inayohusisha mfumo mkuu wa neva. Unaweza kutokea mapema, ikiwa aidha isiyo kuwa na dalili ya ugonjwa au ya kusababisha kaswende meninjitisi; au inaweza kuchelewa, kama kaswende ya veni za tando za ubongo, paresi ya jumla, au tabesi dorsalisi, ambayo inahusu usawa wa mwili na uchungu mkali kwa limbu za chini. Kaswende ya neva iliyochelewa huja kabisa baada ya miaka minne hadi 25 baada ya maambukizi ya hapo awali. Kaswende ya veni za utando za ubongo hufanana hasa ikiwa haiwezi kuzuiliwa kifafa, na paresi ya jumla hufanana hasa na dimenshia na tabtesi dorsalisi.[4] Pia, kunaweza kuwa na Mboni za Agryll Robertson ambazo ni mboni ndogo kwa macho zinazofinyika mtu anapotazama vitu vilivyokaribu, lakini hayafinyiki zikiwa wazi kwa mwanga mkali.

Kaswende ya moyo na mishipa kwa kawaida hutokea miaka 10 hadi30 baada ya maambukizi ya awali. Tatizo la kawaida kabisa ni ule wa kaswende ya kuvimba kwa aota, ambayo inaweza kusababisha aneurisimi kuundwa.[4]

Ya kuzaliwa nayo

Kaswende ya kuzaliwa nayo inaweza kutokea wakati wa mimba au wa kuzaa. Theluthi-mbili ya watoto wazawa wanazaliwa bila dalili. Dalili ambazo huendelea zaidi ya miaka michache ya kwanza ya maisha ni pamoja na: kunenepa nenepa kwa ini au wengu (70%), upele (70%), joto jingi mwilini (40%), kaswende ya neva (20%), na ugonjwa wa mapafu kuvimba (20%). Ikiwa haita tibiwa, kaswende ya kuzaliwa ya baadae inaweza kutokea kwa 40 %, ikiwa ni pamoja na: pua lenye umbo la tandikoulemavu, Higoumenakis sign, saber shin, au Clutton's joints, miongoni mwa zingine.[12]

Chanzo

Bakteriolojia

Histopatholojia ya Treponema pallidum spirosheti zinazotumia kifaa chembamba cha kutia waa cha kisasa

Kigezo:Treponema pallidum Treponema pallidum Kundi la spishi pallidum ni wa umbo-la mzunguko, Gramu-hasi, Bakteria inayosambazika kwa kasi.[8][13]Magonjwa mengine matatu ya binadamu husababishwa na zinazohusiana na Treponema pallidum, ikiwa ni pamoja na buba (kundi la spishi pertenue), pinta(kundi la spishi carateum), na bejel (kundi la spishi endemicum).[4] Tofauti na aina ya pallidum haya hayasababishi ugonjwa wa neva.[12] Wanadamu tu ndio wanaojulikana kuwa na hifadhi asili kwa kundi la spishi pallidum.[5] Bakteria hii haiwezi kuishi bila kimelea. Hii ni kwa sababu ya jenomu yake ndogo (1.14 MDa)na hivyo basi haitaweza kutengeneza virutubishi vikuu. Ina wakati mfupi wa kujiongeza zaidi ya saa 30.[8]

Maambukizi

Kaswende huambukizwa kimsingi kwa kupitia ngono ujauzito kutoka kwa mama hadi kwa fetasi; spirosheti huweza kupitia ukiwa mzima kwa membreni ya utetelezi au ngozi yenye haina kinga.[4][5] na hivyo husambazwa kwakubusu, pia mdomo kwa, uke, na tupu ya nyuma wakati wa ngono.[4] Takriban 30% hadi 60% kwa wale wako wazi kwa hatua ya kwanza au ya pili ya kaswende watapata ugonjwa huo.[11] Maambukizi ya kaswende imefananishwa na ukweli kwamba mtu ambaye amechanjwa na mshushio 57 pekee ana nafasi 50% ya kuambukizwa.[8] Nyingi ya (60%) hali mpya Marekani hutokea kwa wanaume ambao hufanya ngono na wanaume wengine. Kaswende inaweza kusambazwa kupitia vifaa vya damu. Hata hivyo, bidhaa za damu hupimwa kama kuna kaswende katika nchi nyingi, na hivyo hatari hupunguka. Hatari ya maambukizi kutoka kwa kugawana sindano imeonekana kuwa ni chache.[4] Kaswende haiwezi kusambazwa kwa kupitia makalio ya choo, shughuli za kila siku, beseni ya maji moto, au kugawana vyombo vya kukulia au mavazi.[14]

Utambuzi

Bango ya kupima kaswende, inaonyesha mwanamke na mwanaume wakiinamisha vichwa vyao kwa aibu (ca. 1936)

Ni vigumu kutambua kaswende kwa kliniki mapema katika uwasilishaji wake.[8] Uthibitisho wake hufanywa aidha kupitia kupima damu au moja kwa moja kukagua kwa kupitia uchunguzi kwa kutumia hadubini. Kwa kawaida vipimo vya damu hutumika, kwa sababu hutambulika kwa urahisi zaidi.[4] Vipimo vya kutambua ugonjwa haziwezi, hata hivyo, hutofautisha kati ya hatua ya ugonjwa.[15]

Kupima damu

Kupimwa kwa damu hugawanywa katika nontreponemal na vipimo vya treponemal .[8] Vipimo vya Nontreponemal hutumika hapo awali, na ni pamoja na utafiti wa ugonjwa wa zinaa maabarani na vipimo vya Kuongeza ghafla tena kwa plasma. Hata hivyo, kwa vile vipimo hivi ni vya mara kwa maramatukio chanya,uthibitisho inahitajika kwa kupima treponemal, kama vile treponemal pallidum particle agglutination au Uchunguzi wa ufonyzaji wa antibodi ya treponemal iliyo na mwangaza (FTA-Abs).[4] matukio chanya usiokuwa ya ukweli katika uchuguzi wa usio kuwa wa treponemal inaweza kutokea na maambukizi fulani ya virusi kama vile tetekuwanga na ukambi, pia inaweza kutokea na limfoma, kifua kikuu, malaria,uvimbemoyo, ugonjwa wa kuungana kwa tishu, na mimba.[7] Vipimo vya antibodi vya treponemal kawaida huwa chanya baada ya wiki mbili hadi tano ya maambukizi ya hapo awali.[8] Kaswende ya neva hutambulika kwa kupata idadi ya juu ya lukosaiti (kuzidilimfositi) na kiwango cha juu cha protini viowevu vya ubongo na uti wa mgongo katika mazingira ya kaswende inayojulikana.[4][7]

Uchunguzi wa moja kwa moja

Eneo la giza linalochunguzwa kwa kutumia hadubini ya viowevu vya seramu kutoka shanka inaweza kutumika kwa kufanya utambuzi wa haraka.Hata hivyo, sio kawaida kupata vifaa au wakazi wenye ujuzi hospitalini, na vipimo hivi lazima vifanywe kati ya dakika  10 ya kupata sampuli. Kiwango cha hisi kimeripotiwa kuwa takriban 80%, hivyo vipimo hivi vinaweza kutumika tu kuthibitisha utambuzi, lakini si kwa kuchuja moja nje. Vipimo vingine viwili vina weza kufanywa kwa sampuli iliyo toka kwa shanka ni antibodi ya mwangaza ya moja kwa moja na asidi ya kiini . antibodi ya floresini ya njia ya moja kwa moja antibodizilizobandikwa nafloresini, ambayo inajishikilia kwa protini maalum za kaswende. Asidi ya kiini hutumia ufundisanifu, kama vile msururu wa athari za polima, kutambua uwepo wa jeni maalum ya kaswende. Uchunguzi hizi sio shida kwa wakati kama makroskopu inayotumia giza, kwa sababu bakteria hahitajiki ili kufanya utambuzi.[8]

Udhibiti

As of 2010,Hakuna chanjo inayofaa ya kudhibiti. [5] Kujiepusha na uhusiano wa kindani wa kimwili na mtu aliyeambukizwa ni shahihi kwa kupunguza maambukizi ya kaswende, kama ilivyo kwa matumizi sahihi ya kondomu. Matumizi ya kondomu, hata hivyo,hayaondoi kabisa hatari.[16][14] Hivyo, Vituo vya kudhibiti na kuzuia magonjwavinapendekeza uhusiano wa muda-mrefu, kwa kushirikiana na mtu mmoja hajaambukizwa na kujiepusha na vitu kama pombe na dawa zingine ambazo huongeza hatari za kufanya ngono kiholela.[14]

Kaswende ya kuzaliwa nayo katika wazawa inaweza kuzuiwa kwa kuchunguzi mama mapema wakati wa ujauzito na kutibu wale ambao wameambukizwa.[17] Muungano wa Wahudumu wa kutoa udhibiti Merikani inapendekeza sana uchunguzi kwa wanawake wote wajawazito,[18] Shirika la Afya Duniani inapendekeza wanawake wote kupimwa mara ya kwanza wakitembelea kliniki(kabla ya kujifungua)na tena katikakipindi cha tatu cha ujauzito.[19] Iwapo vipimo vinaonyesha uwepo wa ungojwa,inapendekezwa washirika wa akina mama hawa pia watibiwe.[19]. Kaswende ya kuzaliwa nayo, hata hivyo, bado iko kawaida katika inch zinazoendelea, kwa kuwa wanawake wengi hawapati huduma ya kliniki ya wajauzito > kabisa, na wengine huduma ya kliniki ya wajawazito wanayopata haijumulishi uchunguzi wa kaswende.[17] Kaswende ya kuzaliwa nayo huaipatikani mara kwa mara katika nchi zilizoendelea, kwa sababu wale wanaoweza kupata kaswende (kupitia matumizi ya dawa, n.k) pia wako uwezo mdogo zaidi wa kupata huduma wakati wa ujauzito.[17] Hatua zingine za kuongezea upatikanaji wa kupimwa huonekana kuwa na ufanisi katika kupunguza viwango vya kaswende ya kuzaliwa nayo katika chini zilizo na mapato ya chini na ya kati.[19]

Kaswende ni ugonjwa inayohitaji kutolewa taarifa katika nchi nyingi, ikiwa ni pamoja na Canada,[20] Umoja wa Ulaya,[21] na Marikani.[22] Hii inamaanisha kuwa wahuduma wa Afya wanatakiwa kutoa taarifa kwawizara ya Afya ambayo itatoa taarifa kwa washirika hadi kwa washirika wa watu. [23] Madaktari pia wanaweza kuhimiza wagonjwa kutumia washirika wao kupata huduma.[24] Kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa kinapendekeza kwamba wanaume wanaoshiriki ngono na wanaume wengine lazima wapimwe angalau kila mwaka.[25]

Matibabu

Maambukizi ya mapema

Chaguo la kwanza kwa matibabu ya kaswende isiyo na tatizo bado tu ni dosi kimoja ya shindano kwa misulipenisilini G au dosi moja ya dawa ya kumezaazithromycin.[26]Doksiklini na tetrasaiklini ni chaguo mbadala; hata hivyo, hazitumiki kwa akina mama wajawazito. Pingamizi kwa antibiotikiimetokezea kwa baadhi ya maajenti, ikiwa ni pamoja na makrolidi, klindamisini, na rifampini.[5] seftriaksoni, sephalosporini-za tokeo la tatu antibiotiki, zinaweza kufanya kazi kama penisilini kulingana na matibabu.[4]

Maambukizi ya baadaye

Kwa kaswende kwa sababu ya uingiaji duni wa penisilini G kwenye mfumo mkuu wa neva, watu walioathiriwa wanashauriwa kupewa dosi kubwa za penisilini kwa mshipa kwa muda usiopungua siku 10 .[4][5] Iwapo mtu ana aleji ya penisilini, seftriaksoni inaweza kutumiwa, au utoaji wa aleji ya penisilini unaweza kujaribiwa. Zinaotokea baadaye zinaweza kutibiwa na shidano ya penisilini G kwa misuli mara moja-kwa wiki kwa muda wa wiki tatu. Ikiwa mgonjwa ana aleji, doksikilini au tetrasaikilini zinaweza kutumiwa, lakini kwa muda mrefu.Matibabu kwa wakati huu huzuia uendeleaji wa ugonjwa, lakini ina mabaadiliko madogo tu kwa madhara yenye tayari yametokea.[4]

Athari ya Jarisch-Herxheimer

Moja wapo ya athari inayoweza kutokana na matibabu ni athari aina ya Jarisch-Herxheimer. Mara nyingi inaanza ndani ya saa moja baada ya matibabu na hudumu kwa masaa 24, kukiwa na dalili za joto nyingi mwilini, maumivu kwa misuli, maumivu ya kichwa, na takikadia.[4] Inasababishwa na saitokini zinazotolewa na mfumo wa kinga kutokana na lipoprotini zinazotolewa wakati bakteria za kaswende zinazopasuka.[27]

Epidemiolojia

Age-standardized death from syphilis per 100,000 inhabitants in 2004[28]
     no data      <35      35-70      70-105      105-140      140-175      175-210
     210-245      245-280      280-315      315-350      350-500      >500

Inaaminiwa kuwa kaswende iliathiri watu milioni 12 mwaka wa 1999, 90% ya maambukizi yakiwa kwa nchi zinazoendelea.[5] Huathiri kati ya mimba 700,000 na milioni 1.6  kwa mwaka, na kusababisha kuharibika kwa mimba bila hiaris, kuzaa mtoto aliyekufa na kuzaliwa na kaswende. Katikasub-Saharan Africa, kaswende huchangia takriban 20% ya vifo vya watoto wakati wa kuzaliwa.[12] Viwango viko juu zaidi vikilinganishwa na wanaojidunga dawa kwa mshipa, walio na maambukizi ya VVU, na wanaume wanaofanya ngono na wanaume wengine.[29][30][31] Nchini Marekani viwango vya kaswende mno mwaka wa 2007 vilikuwa mara sita zaidi kwa wanaume kuliko ya Wanawake, hata ingawa viwango hivi vilikuwa karibu sawa mwaka wa 1997.[32] Wafrika Wamarika walichangia kwa takriban nusu ya walioambukizwa mwaka wa 2010.[33]

Kaswende ilikuwa ni kawaida nchini Ulaya wakati wa karne ya 18 na 19. -!>. Katika nchi zilizoendelea mwanzo wa karne ya 20, maambukizi yalipungua kwa haraka kwa sababu ya ongezeko la matumizi ya antibiotiki, hadi miaka ya 1980 na 1990.[13] Tangu mwaka wa 2000, viwango vya kaswende vimeongezeka nchini Marekani, Uingereza, Australia na Ulaya, hasa kati ya wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume wengine.[5] viwango vya kaswende miongoni mwa wanawake wa Marekani, hata hivyo,imebakia sawa wakati huu, na viwango kati ya wanawake Uingereza vimeongezeka, lakini katika kiwango cha chini kuliko kile cha wanaume.[34] Ongezeko kwa viwango miongoni mwa wapenzi wa jinsia tofauti ilitokea China na Urusi tangu miaka ya 1990.[5] Hii imehusishwa na mazoea ya kufanya mapenzi bila kinga, kuwa na wapenzi wengi, ukahaba, na upunguvu wa matumizi ya kinga kama vile kondomu.[5][35][34]

Bila kutibiwa, kaswende inasababisha vifo kwa 8% hadi 58%,kiwango kikubwa ikiwa kwa wanaume.[4] Dalili za kaswende zimepunguka kwa ukali katika karne ya 19 na 20 ,kwa sababu ya ueneaji na upatikanaji wa matibabu yanayofaa, na pia kupungua kwaukali wa spirochaete.[9] Ikitibiwa mapema, matatizo chache hutokea.[8] Kaswende huongeza hatari ya maambukizi ya VVU kwa mara 2-5, na yale yanayoambatana ni ya kawaida (30-60% kwa baadhi ya vituo vya mijini).[4][5]

Historia

Portrait of Gerard de Lairesse na Rembrandt van Rijn, ca. 1665–67, oil on canvas. De Lairesse,mwenyewe ni mchoraji na mwanasanaa, aliathiriwa na kaswende kutoka kuzaliwa iliyomwaribu uso wake na hatimaye ikasababisha upofu kwake[36]

Mwanzo halisi wa kaswende haijulikani [4] Kuna nadharia tete mbili za kimsingi:. Moja inapendekeza kuwa kaswende ililetwa Ulaya na wafanyikazi wa meli kutoka Christopher Columbus safari kuelekea Marikani, na nyingine inapendekeza kwamba kaswende ilikuwepo Ulaya hapo awali, lakini haikuwa imetambuliwa. nadharia hizi hujulikana kama nadharia "Columbian" na "kabla ya Columbian", mtawalio.[15] Nadharia ya Columbia inathibitiswa na ushahidi uliopo.[37] Taarifa ya kwanza iliyoandikwa kuhusu mlipuko wa kaswende katika Ulaya iliyotokea katika mwaka wa 1494/1495 katikaNaples, Italia, wakati waliingiliwa na Ufaransa.[13][15] Kutokana na kuenezwa na kundi la wapiganaji wafaransa waliporudi, hapo awali ilijulikana kama "ugonjwa wa Kifaransa". Mwaka wa 1530, jina "kaswende" lilitumiwa kwanza na daktari Mwitaliano na mshairi GirolamoFracastoro kama kichwa chaKilatini shairi lake kuelezea ongezeko la ugonjwa huo Italia.[38] Kaswende pia ilijulikana kihistoria kama "Poksi Kuu".[39][40]

Viumbe vinavyosababishi, Treponema pallidumu, vilitambuliwa kwa mara ya kwanza na Fritz Schaudinn na Erich Hoffmann mwaka wa 1905. [13] matibabu yaliyofaa ya kwanza(Salvarsan) yalitengezwa mwaka wa 1910 na Paul Ehrlich, ambayo ilifuatiliwa na majaribio ya [[penisilini ]] na uthibitisho wa ufanisi wa dawa hiyo mwaka wa 1943 [13][39] Kabla ya kuwepo kwa matibabu yaliyofaa, mercury na kwa kawaida utengaji ulitumika mara nyingi, pamoja na matibabu yaliyokuwa mara nyingi mbaya zaidi kuliko ugonjwa [39] Watu wengi maarufu wa kihistoria, ikiwa ni pamoja na Franz Schubert,Arthur Schopenhauer, ÉdouardManet[13] and Adolf Hitler,[41] waliaminika kuwa walikuwa na ugonjwa huo.

Jamii na Utamaduni

Sanaa na Fasihi

The earliest known medical illustration of patients suffering from syphilis, Vienna, 1498

Sanamu ya kwanza Ulaya iliyoonyesha kaswende ni yaAlbrecht Dürer Mtu aliye kuwa na Kaswende, sanamu ilioyo katwa kutoka kwa mti aliaminika kuonyeza Landsknecht, mtu wa kutoka Ulaya kaskazinikufanya kwa lengo la pesa.[42] kisasili chafemme fatale au "Wanawake sumu" wa karne ya 19 inaaminika kuwa ilitokana na uharibifu wa kaswende, ikiwa na mifano maarufu katika maelezo pamoja na John Keats' La Belle Dame sans Merci.[43][44]

Msanii Jan van der Straet alichora mtu tajiri akipokea matibabu ya kaswende kwenye mti wa tropiki guaiacum hapo karibu mwaka wa 1580.[45] Kichwa cha kazi hiyo ni "Maandalizi na Matumizi ya Guayaco kwa Kutibu Kaswende".Kwa kuwa msanii alichagua kuweka picha hii kwa kazi zilizofuatana za kuadhimisha Dunia mpya inayoonyesha umuhimu wa matibabu ya kaswende, hata ingawa yasiofaa, ya kaswende ulivyokuwa kwa wasomi wa Ulaya wakati huo. Mchoro uliyokuwa na rangi nyingi na tondoti inaonyesha wafanyi kazi wanne wakiandaa mchanganyiko huo wakati daktari akiangalia, akiwa ameficha kitu nyuma wakati mgonjwa hasio bahatika anakunywa.[46]

Utafita wa Tuskegee na Guatemala

Moja ya hali iliyokuwa na sifa mbaya Merikani kuhusumaadili ya kimatibabu katika karne ya 20 ilikuwa niUtafiti wa kaswende ya Tuskegee.[47] Utafiti ulifanywaTuskegee, Alabama, ili fadhiliwa naHuduma ya afya ya umma Marikani (PHS) ikisaidiana naTaasisi ya Tuskegee.[48] Utafiti huu ulianza mwaka wa 1932, wakati kaswende ilikuwa tatizo sana na hakukuwa na matibabu yaliyofaa na salama.[6] Utafiti huo ulinia kupima Maendeleo ya kaswende bila matibabu. Kufikia 1947, penisilini ilikuwa imekubaliwa kuwa ndio tiba sahihi kwa matibabu yaliofaa kwa kaswende na ilikuwa ikitumika sana kwa kutibu ugonjwa huo. <-! CDCTime ->Wakurugenzi wa utafiti huu, hata hivyo, waliendelea na utafiti na hawakuwapa washiriki matibabu na penisilini. [48]hiiimejadiliwa, na baadhi yao wamegundua kwamba penisilini alipewa washirika wengi<ref. name="TUS00"/>Utafiti haukuisha hadi 1972.[48]

Majaribio ya kaswende pia yalifanywa katikaGuatemala kutoka 1946 hadi 1948. Yalikuwa yamefadhiliwa namarikani [[|utafiti kwa binadamu|majaribio kwa binadamu]], yaliyofanywa wakati wa serikali ya Juan José Arévalo ikiwa na ushirikiano na baadhi ya wizara za afya na maafisa wa Guatemala. Madaktari waliambukiza askari, wafungwa, na wagonjwa wa akili na kaswende na magonjwa menginemagojnwa ya zinaa, bila ridhaa ya washiriki, na kisha kuwatibi na antibiotiki. Mwezi wa Oktoba 2010, Marekani iliomba msamaha rasmi kwa Guatemala kwa kufanya majaribio haya.[49]

Tanbihi

  1. Coffin, LS (2010 Jan). "Syphilis in Drug Users in Low and Middle Income Countries". The International journal on drug policy. 21 (1): 20–7. doi:10.1016/j.drugpo.2009.02.008. PMC 2790553. PMID 19361976. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  2. Gao, L (2009 Sep). "Meta-analysis: prevalence of HIV infection and syphilis among MSM in China". Sexually transmitted infections. 85 (5): 354–8. doi:10.1136/sti.2008.034702. PMID 19351623. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  3. Karp, G (2009 Jan). "Syphilis and HIV co-infection". European journal of internal medicine. 20 (1): 9–13. doi:10.1016/j.ejim.2008.04.002. PMID 19237085. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  4. 4.00 4.01 4.02 4.03 4.04 4.05 4.06 4.07 4.08 4.09 4.10 4.11 4.12 4.13 4.14 4.15 4.16 4.17 4.18 4.19 4.20 4.21 4.22 4.23 4.24 4.25 4.26 4.27 4.28 4.29 Kent ME, Romanelli F (2008). "Reexamining syphilis: an update on epidemiology, clinical manifestations, and management". Ann Pharmacother. 42 (2): 226–36. doi:10.1345/aph.1K086. PMID 18212261. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
  5. 5.00 5.01 5.02 5.03 5.04 5.05 5.06 5.07 5.08 5.09 5.10 Stamm LV (2010). "Global Challenge of Antibiotic-Resistant Treponema pallidum" (PDF). Antimicrob. Agents Chemother. 54 (2): 583–9. doi:10.1128/AAC.01095-09. PMC 2812177. PMID 19805553. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2014-04-25. Iliwekwa mnamo 2013-11-28. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help); Unknown parameter |month= ignored (help)
  6. 6.0 6.1 White, RM (2000-03-13). "Unraveling the Tuskegee Study of Untreated Syphilis". Archives of internal medicine. 160 (5): 585–98. doi:10.1001/archinte.160.5.585. PMID 10724044.
  7. 7.0 7.1 7.2 7.3 Committee on Infectious Diseases (2006). Larry K. Pickering (mhr.). Red book 2006 Report of the Committee on Infectious Diseases (tol. la 27th). Elk Grove Village, IL: American Academy of Pediatrics. ku. 631–44. ISBN 9781581102079.
  8. 8.00 8.01 8.02 8.03 8.04 8.05 8.06 8.07 8.08 8.09 8.10 8.11 8.12 Eccleston, K (2008 Mar). "Primary syphilis". International journal of STD & AIDS. 19 (3): 145–51. doi:10.1258/ijsa.2007.007258. PMID 18397550. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  9. 9.0 9.1 9.2 Mullooly, C (2010 Aug). "Secondary syphilis: the classical triad of skin rash, mucosal ulceration and lymphadenopathy". International journal of STD & AIDS. 21 (8): 537–45. doi:10.1258/ijsa.2010.010243. PMID 20975084. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  10. Dylewski J, Duong M (2 Januari 2007). "The rash of secondary syphilis". Canadian Medical Association Journal. 176 (1): 33–5. doi:10.1503/cmaj.060665. PMC 1764588. PMID 17200385.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. 11.0 11.1 11.2 11.3 11.4 11.5 11.6 Bhatti MT (2007). "Optic neuropathy from viruses and spirochetes". Int Ophthalmol Clin. 47 (4): 37–66, ix. doi:10.1097/IIO.0b013e318157202d. PMID 18049280.
  12. 12.0 12.1 12.2 Woods CR (2009). "Congenital syphilis-persisting pestilence". Pediatr. Ambukiza. Dis. J. 28 (6): 536–7. doi:10.1097/INF.0b013e3181ac8a69. PMID 19483520. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
  13. 13.0 13.1 13.2 13.3 13.4 13.5 Franzen, C (2008 Dec). "Syphilis in composers and musicians--Mozart, Beethoven, Paganini, Schubert, Schumann, Smetana". European Journal of Clinical Microbiology and Infectious Diseases. 27 (12): 1151–7. doi:10.1007/s10096-008-0571-x. PMID 18592279. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help)
  14. 14.0 14.1 14.2 "Syphilis - CDC Fact Sheet". Centers for Disease Control and Prevention (CDC). 16 Septemba 2010. Iliwekwa mnamo 2007-05-30.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  15. 15.0 15.1 15.2 Farhi, D (2010 Sep-Oct). "Origins of syphilis and management in the immunocompetent patient: facts and controversies". Clinics in dermatology. 28 (5): 533–8. doi:10.1016/j.clindermatol.2010.03.011. PMID 20797514. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  16. Koss CA, Dunne EF, Warner L (2009). "A systematic review of epidemiologic studies assessing condom use and risk of syphilis". Sex Transm Dis. 36 (7): 401–5. doi:10.1097/OLQ.0b013e3181a396eb. PMID 19455075. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  17. 17.0 17.1 17.2 Schmid, G (2004 Jun). "Economic and programmatic aspects of congenital syphilis prevention". Bulletin of the World Health Organization. 82 (6): 402–9. PMC 2622861. PMID 15356931. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help)
  18. U.S. Preventive Services Task, Force (2009 May 19). "Screening for syphilis infection in pregnancy: U.S. Preventive Services Task Force reaffirmation recommendation statement". Annals of internal medicine. 150 (10): 705–9. PMID 19451577. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help)
  19. 19.0 19.1 19.2 Hawkes, S (2011 Jun 15). "Effectiveness of interventions to improve screening for syphilis in pregnancy: a systematic review and meta-analysis". The Lancet infectious diseases. 11 (9): 684–91. doi:10.1016/S1473-3099(11)70104-9. PMID 21683653. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  20. "National Notifiable Diseases". Public Health Agency of Canada. 2005-04-05. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-08-09. Iliwekwa mnamo 2 Agosti 2011.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  21. Viñals-Iglesias, H (2009 Sep 1). "The reappearance of a forgotten disease in the oral cavity: syphilis". Medicina oral, patologia oral y cirugia bucal. 14 (9): e416–20. PMID 19415060. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  22. "Table 6.5. Infectious Diseases Designated as Notifiable at the National Level-United States, 2009 [a]". Red Book. Iliwekwa mnamo 2 Agosti 2011.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  23. Brunner & Suddarth's textbook of medical-surgical nursing (tol. la 12th). Philadelphia: Wolters Kluwer Health/Lippincott Williams & Wilkins. 2010. uk. 2144. ISBN 9780781785891.
  24. Hogben, M (2007 Apr 1). "Partner notification for sexually transmitted diseases". Clinical infectious diseases: an official publication of the Infectious Diseases Society of America. 44 Suppl 3: S160–74. doi:10.1086/511429. PMID 17342669. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help)
  25. "Trends in Sexually Transmitted Diseases in the United States: 2009 National Data for Gonorrhea, Chlamydia and Syphilis". Centers for Disease Control and Prevention (CDC). 22 Novemba 2010. Iliwekwa mnamo 3 Agosti 2011.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  26. David N. Gilbert, Robert C. Moellering, George M. Eliopoulos; na wenz. The Sanford guide to antimicrobial therapy 2011 (tol. la 41st). Sperryville, VA: Antimicrobial Therapy. uk. 22. ISBN 9781930808652. {{cite book}}: Explicit use of et al. in: |author= (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  27. Radolf, JD; Lukehart SA (editors) (2006). Pathogenic Treponema: Molekiuli na bayolojia ya chembechembe. Caister Academic Press. ISBN 1-904455-10-7. {{cite book}}: |author= has generic name (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  28. "Disease and injury country estimates". World Health Organization (WHO). 2004. Iliwekwa mnamo 11 Novemba 2009.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  29. Coffin, LS (2010 Jan). "Syphilis in Drug Users in Low and Middle Income Countries". The International journal on drug policy. 21 (1): 20–7. doi:10.1016/j.drugpo.2009.02.008. PMC 2790553. PMID 19361976. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  30. Gao, L (2009 Sep). "Meta-analysis: prevalence of HIV infection and syphilis among MSM in China". Sexually transmitted infections. 85 (5): 354–8. doi:10.1136/sti.2008.034702. PMID 19351623. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  31. Karp, G (2009 Jan). "Syphilis and HIV co-infection". European journal of internal medicine. 20 (1): 9–13. doi:10.1016/j.ejim.2008.04.002. PMID 19237085. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  32. "Trends in Reportable Sexually Transmitted Diseases in the United States, 2007". Centers for Disease Control and Prevention(CDC). 13 Januari 2009. Iliwekwa mnamo 2 Agosti 2011.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  33. "STD Trends in the United States: 2010 National Data for Gonorrhea, Chlamydia, and Syphilis". Centers for Disease Control and Prevention (CDC). 22 Novemba 2010. Iliwekwa mnamo 20 Novemba 2011.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  34. 34.0 34.1 Kent, ME (2008 Feb). "Reexamining syphilis: an update on epidemiology, clinical manifestations, and management". The Annals of pharmacotherapy. 42 (2): 226–36. doi:10.1345/aph.1K086. PMID 18212261. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  35. Ficarra, G (2009 Sep). "Syphilis: The Renaissance of an Old Disease with Oral Implications". Head and neck pathology. 3 (3): 195–206. doi:10.1007/s12105-009-0127-0. PMC 2811633. PMID 20596972. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  36. The Metropolitan Museum of Art Bulletin, Summer 2007, pp. 55–56.
  37. Rothschild, BM (2005-05-15). "History of syphilis". Clinical infectious diseases: an official publication of the Infectious Diseases Society of America. 40 (10): 1454–63. doi:10.1086/429626. PMID 15844068.
  38. Nancy G. "Siraisi, Drugs and Diseases: New World Biology and Old World Learning," in Anthony Grafton, Nancy G. raisi, with April Shelton, eds., New World, Ancient Texts (Cambridge MA: Belknap Press/Harvard University Press, 1992), 159-94
  39. 39.0 39.1 39.2 Dayan, L (2005 Oct). "Syphilis treatment: old and new". Expert opinion on pharmacotherapy. 6 (13): 2271–80. doi:10.1517/14656566.6.13.2271. PMID 16218887. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  40. Knell, RJ (2004-05-07). "Syphilis in renaissance Europe: rapid evolution of an introduced sexually transmitted disease?" (PDF). Proceedings. Biological sciences / the Royal Society. 271 Suppl 4 (Suppl 4): S174–6. doi:10.1098/rsbl.2003.0131. PMC 1810019. PMID 15252975.
  41. "Hitler syphilis theory revived", BBC News, 12 March 2003. 
  42. Eisler, CT (2009 Winter). "Who is Dürer's "Syphilitic Man"?". Perspectives in biology and medicine. 52 (1): 48–60. doi:10.1353/pbm.0.0065. PMID 19168944. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help)
  43. Hughes, Robert (2007). Things I didn't know : a memoir (tol. la 1st Vintage Book). New York: Vintage. ku. 346. ISBN 9780307385987.
  44. Wilson, [ed]: Joanne Entwistle, Elizabeth (2005). Body dressing (tol. la [Online-Ausg.]). Oxford: Berg Publishers. uk. 205. ISBN 9781859734445. {{cite book}}: |first= has generic name (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  45. Reid, Basil A. (2009). Myths and realities of Caribbean history (tol. la [Online-Ausg.]). Tuscaloosa: University of Alabama Press. uk. 113. ISBN 9780817355340.
  46. "Preparation and Use of Guayaco for Treating Syphilis" Archived 21 Mei 2011 at the Wayback Machine.. Jan van der Straet. Retrieved 6 August 2007.
  47. Katz RV, Kegeles SS, Kressin NR; na wenz. (2006). "The Tuskegee Legacy Project: Willingness of Minorities to Participate in Biomedical Research". J Health Care Poor Underserved. 17 (4): 698–715. doi:10.1353/hpu.2006.0126. PMC 1780164. PMID 17242525. {{cite journal}}: Explicit use of et al. in: |author= (help); Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  48. 48.0 48.1 48.2 "U.S. Public Health Service Syphilis Study at Tuskegee". Centers for Disease Control and Prevention (CDC). 15 Juni 2011. Iliwekwa mnamo 2010-07-07.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  49. "U.S. apologizes for newly revealed syphilis experiments done in Guatemala", The Washington Post, 1 October 2010. Retrieved on 1 October 2010. "The United States revealed on Friday that the government conducted medical experiments in the 1940s in which doctors infected soldiers, prisoners and mental patients in Guatemala with syphilis and other sexually transmitted diseases."