iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.
iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.



Link to original content: https://sw.wikipedia.org/wiki/Chelezo
Chelezo - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Chelezo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Vyelezo kwenye mto Volga, Urusi, mnamo 1913.
Chelezo cha Kon-Tiki mwaka 1947.
Chelezo kwenye milima ya Pirenei, Ufaransa.

Chelezo ni chombo sahili cha usafiri kwenye maji. Kinafanywa na vitu vinavyoweza kuelea juu ya maji vinavyofungwa pamoja ili kuwa na uso bapa ambako watu wanaweza kukaa na kusafiri kwenye maji.

Chelezi asilia

[hariri | hariri chanzo]

Kiasili chelezo ni vipande vya miti vilivyofungwa pamoja kwa kamba. Watu walitumia vyombo vya aina hii tangu kale kuvuka mito lakini pia kusafiri baharini.

Penye mito mikubwa ubao ulisafirishwa mara nyingi kwa njia ya chelezo ilhali miti iliyokatwa iliunganishwa pamoja na kuendeshwa na watu kwa kufuata mwendo wa maji hadi kufika kwenye shabaha yake yaani penye wateja. Chelezo sahili kinakwenda tu na mwendo wa maji.

Jaribio la chelezo Kon-Tiki

[hariri | hariri chanzo]

Inawezekana pia kuendesha chelezo kwa kutumia usukani na tanga. Mwaka 1947 Thor Heyerdahl (mtaalamu wa anthropolojia kutoka nchi ya Norwei) alionyesha kwamba inawezekana kuvuka Bahari Pasifiki kwa chelezo. Heyerdahl alitengeneza chelezo kwa kutumia ubao mwepesi aina ya balsa alichoita Kon-Tiki kufuatana na taarifa za kale akaanza safari kwenye pwani ya Peru na baada ya siku 101 alifika kwenye kisiwa cha Polynesia ya Kifaransa kusini mwa Pasifiki. Aliweza kulenga chelezo kiasi kwa msaada wa usukani, hivyo alionyesha kwamba chelezo hakitegemei upepo na mikondo ya bahari pekee, na kamba chelezo kinachotegnezewa pekee kwa ubao na kamba inaweza kudumu miezi.

Vyelezo vya vifaa vya kisasa

[hariri | hariri chanzo]

Tangu kupatikana kwa mata za kikemia na chuma vyelezo hutengenezwa pia kwa kutumia

  • plastiki nyepesi inayoelea juu ya maji
  • vyombo kama mapipa vyenye hewa ndani yake vinavyoweza kubeba mizigo mizito kushinda ubao.

Viungu vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Simple English Wiktionary
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
Wikimedia Commons ina media kuhusu: