iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.
iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.



Link to original content: https://sw.wikipedia.org/wiki/Black_Kei_River
Black Kei River - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Black Kei River

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Black Kei River iko Afrika Kusini

Mto Black Kei ni mto wa Afrika Kusini wenye chanzo chake kusini magharibi mwa mji wa Queenstown, katika Rasi ya Mashariki. Unaendelea kuishia katika mto White Kei, na kuunda mto wa Great Kei.

Vijiji mbalimbali viko karibu na pembezoni mwa mto huo; vijiji hivyo ni kama: McBride, Qabi, Ntabelanga, Thornhill, Tsolwana Thornhill, Loudon, Tsolwana Loudon, Mitford, Ghuba ya Mashariki Mitford, Basoto, Tsolwana Basoto, shamba kubwa la Baccle na Tentergate.

Kuna lambo moja linalounda bwawa la kuhifadhia maji. Kwa sasa mto huu ni sehemu ya ukusanyaji na Uhifadhi wa maji wa Mzimvubu mpaka Keiskama.[1]

Sehemu yake ya juu huunda mpaka wa magharibi wa Hifadhi Asili ya Tsolwana, na wakati wa kipindi cha kati ya miaka ya 1800, Black Kei na tawimto lake Klipplaat vilitengeneza mpaka wa kaskazini wa British Kaffraria.

Mto Klaas, Klaas Smits na Mto Klipplaat ndiyo matawi makuu ya mto huu.[2]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Black Kei River kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.