iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.
iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.



Link to original content: https://sw.wikipedia.org/wiki/Beijing
Beijing - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Beijing

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru








Jiji la Beijing
Faili:Flag of .png
Bendera
Nchi Uchina
Beijing

Beijing (pia: Peking) ni mji mkuu wa China. Iko kaskazini-mashariki mwa nchi. Rundiko la jiji lina wakazi wapitao milioni 15.

Tangu karne sita imekuwa kitovu cha utawala wa China. Jina lenyewe lamaanisha "Mji Mkuu wa Kaskazini" kwa sababu China iliwahi kuwa na vitovu mbalimbali hasa Nanjing (mji mkuu wa kusini).

Kiutawala jiji la Beijing pamoja na maeneo ya jirani hutawaliwa kama mkoa wa nchi wenye eneo la km² 16,800.

Kutokana na historia ndefu kuna majengo mengi mazuri yanayohifadhiwa hata kama mitaa mingine inabadilika haraka. Sehemu inayohifadhiwa ni pamoja na Uwanja wa Tianamen, Mji Haramu pamoja na nyumba za makaisari wa China na mahekalu mbalimbali.

Leo hii Beijing ni mji mkubwa wa pili katika China baada ya Shanghai. Katika historia iliwahi kuwa mji mkubwa duniani katika karne ya 13 hadi ya 18.

Mwaka 2008 Beijing ilikuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki.


Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Beijing kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.