Yohane Mbatizaji wa Rossi
Mandhari
Yohane Mbatizaji wa Rossi (kwa Kiitalia: Giovanni Battista de' Rossi; Voltaggio, Piemonte, 22 Februari 1698 – Roma, Lazio, 23 Mei 1764) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki nchini Italia.
Papa Pius IX alimtangaza mwenye heri tarehe 13 Mei 1860, halafu Papa Leo XIII akamtangaza mtakatifu tarehe 8 Desemba 1881[1].
Sikukuu yake huadhimishwa katika tarehe ya kifo chake[2].
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Mtoto wa maskini, alikwenda Roma kwa masomo[3] akapewa upadrisho ingawa alikuwa ameanza kuugua kifafa kilichomsumbua hadi mwisho wa maisha yake.
Tangu hapo alijitosa kuhudumia fukara na waliotengwa na jamii, wakiwa pamoja na wanawake, wagonjwa, wafungwa, wafanyakazi, akiwapa pia mafundisho ya Kikristo mbali ya kuadhimisha sakramenti ya upatanisho kwa wengi[4].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "St. John Baptist de Rossi". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913.
- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ https://books.google.com/books?id=g9cUepZUT-IC&pg=PA26 Accessed 14 June 2014; http://mercaba.org/Rialp/J/juan_bautista_de_rossi_san.htm Accessed 14 June 2014
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/54450
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |