iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.
iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.



Link to original content: http://sw.wikipedia.org/wiki/Tajikistan
Tajikistan - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Tajikistan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ҷумҳурии Тоҷикистон
(jumkhurii Tojikiston)

Jamhuri ya Tajikistan
Bendera ya Tajikistan Nembo ya Tajikistan
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: --
Wimbo wa taifa: Surudi Milli
Lokeshen ya Tajikistan
Mji mkuu Dushanbe
38°33′ N 68°48′ E
Mji mkubwa nchini Dushanbe
Lugha rasmi Kitajiki (Kiajemi ya Tajikistan)
Serikali Jamhuri
Emomali Rahmonov
Kokhir Rasulzoda
Uhuru
kutoka Umoja wa Kisoviet
Mwanzo wa Dola la Samaniya

9 Septemba 1991
875 BK
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
143,100 km² (ya 98)
1.8
Idadi ya watu
 - Julai 2019 kadirio
 - 2010 sensa
 - Msongamano wa watu
 
9,275,827 1 (ya 96 1)
7 564 500
48.6/km² (ya 155)
Fedha Somoni (TJS)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+5)
(UTC)
Intaneti TLD .tj
Kodi ya simu +992

-

1.) Rank based on U.N. 2005 figures. Estimate based on CIA figures for 2006.


Tajikistan ni nchi ndogo ya Asia ya Kati ambayo haina pwani kwenye bahari yoyote.

Ramani ya Tajikistan

Imepakana na Uchina, Afghanistan, Uzbekistan na Kyrgyzstan.

Eneo lake ni km² 143,100.

Idadi ya wakazi ni milioni 9.3.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Sehemu kubwa ya nchi ni milima ya Pamir yenye kimo kati ya mita 3600 na 4400.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Kihistoria maeneo ya Tajikistan yalitawaliwa na madola mbalimbali, hasa na Uajemi.

Uislamu ulifika huko mnamo mwaka 800 BK.

Mwaka 1868 Tajikistan ilivamiwa na Urusi na kuwa sehemu ya Dola la Urusi, halafu sehemu ya Umoja wa Kisovyet baada ya mapinduzi ya 1917. Tangu mwaka 1929 iliitwa Jamhuri ya Kisovyet ya Kisoshalisti ya Tajikistan.

Dushanbeː kituo cha reli.

Baada ya kuporomoka kwa Umoja wa Kisoviet, Tajikistan ilipata uhuru wake mwaka 1991.

Kati ya mwaka 1992 hadi 1997 kulikuwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe ambayo ilisababisha Warusi wengi kuondoka na ilikwisha kwa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Baada ya mashambulio ya kigaidi ya tarehe 11 Septemba 2001 jeshi la Marekani lilipata nafasi ya kutumia vituo vya kijeshi kwa ajili ya vita katika Afghanistan.

Wakazi wengi ni Watajiki na kuongea Kitajiki (84.2%), lugha ambayo inahusiana na Kiajemi. Ndiyo lugha rasmi na ya kawaida. Kabila linalofuata kwa ukubwa ni Wauzbeki (13.9%). Angalia pia orodha ya lugha za Tajikistan.

Wananchi wengi ni Waislamu (96.7%), hasa Wasuni, na ndiyo dini rasmi tangu mwaka 2009; Washia ni 3%. Wakristo ni 1.6%, hasa Waorthodoksi na Waprotestanti.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tajikistan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.