Papa Gregori III
Papa Gregori III alikuwa Papa kuanzia tarehe 18 Machi 731 hadi kifo chake tarehe 28 Novemba 741[1].
Alizaliwa katika nchi ya Syria[2], akiwa Papa wa mwisho kutokea nje ya Ulaya hadi alipochaguliwa Papa Fransisko mwaka 2013[3]. Baba yake aliitwa Yohane[4].
Alimfuata Papa Gregori II akafuatwa na Papa Zakaria.
Mara baada ya kuchaguliwa na umati wa waumini [5] na kuthibitishwa na mwakilishi wa kaisari wa Dola la Roma Mashariki[6] alimsihi Kaisari Leo III alegeze msimamo wake wa kupinga matumizi ya picha takatifu. Kwa kuwa balozi wake alikamatwa, Papa aliitisha Sinodi ya Roma (731) iliyolaani vikali msimamo huo[7].
Pamoja na maamuzi mengine, Papa Gregori III alimfanya mmisionari Bonifas kuwa askofu mkuu na balozi wake huko Ujerumani[8]. Vilevile aliunga mkono kazi ya Wilibaldi hukohuko [9]
Alipaswa pia kupambana na uvamizi wa Walombardi katika Italia ya Kati akitegemea kwanza msaada wa kaisari, halafu ule wa Wafaranki, ambao hata hivyo hawakuitikia sana.
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake ni tarehe 10 Desemba[10].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
- Orodha ya Mapapa
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
- ↑ https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
- ↑ "Brusher S.J., Joseph. "St. Gregory III", Popes Through the Ages". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-09-21. Iliwekwa mnamo 2022-04-15.
- ↑ "The Cardinals of the Holy Roman Church". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-05. Iliwekwa mnamo 15 Machi 2013.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Mann, p. 204
- ↑ Levillain, p. 643
- ↑ Treadgold, p. 354; Mann, p. 205
- ↑ Levillain, p. 644
- ↑ Mershman, Francis. "Sts. Willibald and Winnebald." The Catholic Encyclopedia Vol. 15. New York: Robert Appleton Company, 1912. 18 September 2017
- ↑ Martyrologium Romanum
Vyanzo
[hariri | hariri chanzo]- Levillain, Philippe (2002). The papacy : Gaius-Proxies. New York: Routledge. ISBN 9780415922302.
- Duffy, Eamon (2006). Saints & Sinners: A History of the Popes. New Haven, Conn.: Yale University Press. ISBN 9780300115970.
- Treadgold, Warren (1997). A History of the Byzantine State and Society. Stanford, California: Stanford University Press. ISBN 978-0804726306.
- Mann, Horace K. (1914). The Lives of the Popes in the Early Middle Ages. Juz. la I: The Popes Under the Lombard Rule, Part 2, 657–795. ku. 203–224.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Gregori III kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |