Kyushu
Mandhari
(Elekezwa kutoka Kyūshū)
Kyūshū ni kisiwa kikubwa cha tatu nchini Japani na kisiwa cha kusini kati ya visiwa vikubwa vinne vya nchi. Neno kyushu lamaanisha "mikoa tisa" iliyohesabiwa zamani kisiwani.
Idadi ya wakzi ilikuwa 14,779,000 mnamo mwaka 2003.
Kuna milima mingi pamoja na volkeno kama vile mlima Aso (1,592 m) ambayo ni volkeno hai.
Miji muhimu ni Fukuoka, Kitakyūshū na Nagasaki.
Hali ya hewa ni la joto wastani. Mazao ya mpunga, chai, tumbako, viazi na soya hustawi vizuri.