iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.
iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.



Link to original content: http://sw.wikipedia.org/wiki/Kamera_pembuzi
Kamera pembuzi - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Kamera pembuzi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kamera pembuzi nyeusi.

Kamera pembuzi (kwa Kiingereza: webcam) ni kifaa cha tarakilishi kinachotumika kwa kutoa video mtandaoni. Programu ya kamera pembuzi huwawezesha watumiaji kurekodi au kuonyesha video mubashara mtandaoni. Watu wanatumia kamera pembuzi kwa kuongea kama uso kwa uso mtandaoni baina ya watu wawili au zaidi, na maongezi hayo huweza kuwa ya sauti au video mubashara [1] .

Kamera pembuzi kwa kawaida huwa kamera ndogo kwa umbo ambazo huweza kuwekwa juu ya dawati au meza, au katika tarakilishi ya mtumiaji. Vipimo vya ukubwa wa kamera pembuzi huwa ni vidogo kuliko kamera nyingi za kubebwa mikononi, na udogo huo wa umbo hufanya kamera hizo kuwa za gharama ya chini ukilinganisha na kamera nyingi za kurekodi video, hata hivyo udogo huo bado huweza kukidhi maongezi ya video kwa urahisi.

  1. Kwa mfano kamera ya kampuni ya Apple ijulikanayo kama iSight, ambayo imeundiwa katika tarakilishi za Apple za iMacs pamoja na simu kadha za iPhone, zinaweza kutumika kwa ajili ya maongezi ya video, kwa kutumia programu ya kutuma ujumbe wa papo hapo ijulikanayo kama iChat.
  • Miller, D., & Sinanan, J. (2014). Webcam. John Wiley & Sons.
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.