John Glenn
John Herschel Glenn Jr (18 Julai 1921 – 8 Desemba 2016) alikuwa mwanaanga na mwanasiasa kutoka nchini Marekani.
Anajulikana sana kwa kuwa Mmarekani wa kwanza kuzunguka Dunia kwenye mwaka 1962 kama mwanaanga NASA. Baada ya kazi yake kama mwanaanga, aliingia kwenye siasa na aliwahi kuwa Seneta kutoka jimbo lake la Ohio miaka 1974-1999.
Mnamo 1998, alirushwa kwenye anga-nje mara ya pili akiwa na umri wa miaka 77, akijitolea kwa utafiti kuhusu athira ya hali isiyo na graviti kwa wazee. Yeye ndiye mtu wa zamani zaidi katika anga za juu. [1]
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Glenn alizaliwa huko Cambridge, Ohio, akiwa ni mtoto wa John Glenn, Sr. na Teresa Sproat. [2] Alilelewa huko New Concord, Ohio . Glenn alisoma uhandisi katika Chuo cha Muskingum . Alipokea leseni yake ya urubani mnamo 1941. Alipokea Shahada ya Sayansi katika Chuo cha Muskingum.
Rubani wa kijeshi
[hariri | hariri chanzo]Glenn alijiunga na Jeshi la Wanamaji wakati wa Vita Kuu ya Pili mnamo 1942 na kuwa rubani. Baada ya muda mfupi alihamia Jeshi la Marines. Alihudumia kama rubani katika mapignao kwenye Bahari ya Pasifiki.
Glenn alikaa jeshini baada ya vita akashiriki katika Vita ya Korea.
Baada ya vita alikuwa rubani kwa ndege mpya za majaribio. Mnamo Julai 16, 1957 Glenn aliweka rekodi ya kasi akiruka kwenye ndege ya F8U-1 Crusader kutoka Los Angeles hadi New York katika muda wa masaa 3, dakika 23 dakika na sekunde 8.
Mwanaanga
[hariri | hariri chanzo]Mnamo 1958, Glenn alijiunga na Mradi wa Mercury iliyolenga kuandaa safari za kwanza katika anga-nje. Alikuwa mzee kati ya marubani saba waliochaguliwa. Baada ya Alan Shepard na Gus Grissom waliokuwa Wamarekani wa kwanza kurushwa hadi anga-nje kwa safari fupi, Glenn alikuwa Mmarekani wa kwanza aliyezunguka Dunia yote katika anga-nje kwenye tarehe 20 Februari 1962. Umoja wa Kisovyeti ulikuwa umetangulia kwa safari ya Yuri Gagarin aliyewahi kuzunguka Dunia yote tarehe 12 Aprili 1961.
Mwaka 1964 alistaafu kutoka NASA na jeshi .
Alirudi angani mara moja tena mnamo mwaka 1998, akarushwa katika chomboanga space shuttle. Alijitolea kwa majaribio na vipimo mbalimbali vilivyolenga kuangalia athira ya graviti kwa watu wazee.
Mfanyabiashara na mwanasiasa
[hariri | hariri chanzo]Baada ya kustaafu katika NASA alianza biashara yake kwa kampuni ya vinywaji. Mwaka 1974 aligombea nafasi katika bunge ya senati akachaguliwa na kurudishwa hadi kustaafu mwaka 1999.
Maisha binafsi
[hariri | hariri chanzo]Mnamo Aprili 6, 1943, Glenn alioa mpenzi wake wa utoto, Anna Margaret Castor . Walikuwa wamekutana huko New Concord na walicheza pamoja kwenye bendi ya shule. Walizaa wa watoto wawili. Glenn aliishi na mkewe pale Columbus, Ohio .
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ John Glenn: 1st American to Orbit Earth, Oldest Man in Space at Space.com
- ↑ "Archived copy". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-12-21. Iliwekwa mnamo 2013-07-12.
{{cite web}}
: CS1 maint: archived copy as title (link)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- John Glenn Aliheshimiwa kama Balozi wa Uchunguzi Archived 16 Machi 2010 at the Wayback Machine.
- John & Annie Glenn Tovuti ya Historia na Nyumba
- John Glenn Shule ya Masuala ya Umma, Chuo Kikuu cha Jimbo la Ohio Archived 14 Agosti 2015 at the Wayback Machine.
- Wasifu rasmi wa John Glenn wa NASA
- "John Glenn's Flight on Friendship 7, MA-6 – as heard on KCBS Radio". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-10-27.
- Ndege ya John Glenn juu ya Urafiki 7, MA-6 - kamilisha kurekodi sauti ya vidonge vya saa 5
- Ndege ya John Glenn kwenye Shuttle ya Anga, STS-95 Archived 31 Agosti 2006 at the Wayback Machine.
- Wasifu wa Spacefacts wa John Glenn
- Jalada la John Glenn Archived 24 Juni 2010 at the Wayback Machine.
- John Glenn: Picha ambazo hazijachapishwa Archived 23 Desemba 2011 at the Wayback Machine. - onyesho la slaidi na jarida la Life
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu John Glenn kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |