iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.
iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.



Link to original content: http://sw.wikipedia.org/wiki/Historia_ya_Algeria
Historia ya Aljeria - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Historia ya Aljeria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Historia ya Algeria)

Historia ya Aljeria inahusu eneo la Afrika Kaskazini ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Aljeria.

Historia ya kale

[hariri | hariri chanzo]

Historia inayojulikana ilianza na Waberberi ambao wametokana na mchanganyiko wa wakazi asilia.

Tangu mwaka 1000 KK Wafinisia walianza kufika na kujenga miji yao ya biashara kwenye pwani ya Mediteranea. Muhimu zaidi kati ya miji yao ulikuwa Karthago uliopanua utawala wake hadi Uhispania na Gallia (Ufaransa ya Kusini).

Kumbe Waberber wa bara walijenga milki zao za Numidia na Mauretania.

Katika vita kati ya Karthago na Roma ya Kale Waberber walisimama upande wa Roma, hivyo wakapata uhuru wao kwa muda kidogo, lakini wakati wa karne ya 1 KK Roma ilianza kutawala eneo la Aljeria moja kwa moja.

Numidia na Mauretania zilikuwa mashamba ya Roma na sehemu kubwa ya nafaka za Italia zililimwa huko.

Mawe ya maghofu ya miji ya kale bado yanaonyesha uhusiano wa Aljeria na Dola la Roma lililoitawala kwa karne nyingi hadi kuja kwa Waarabu katikati ya karne ya 7.

Utawala wa Roma ulivurugika baada ya Wavandali kutoka Ulaya Kaskazini kufika na kuanzisha milki yao kwa muda wa karne moja.

Jeshi la Kaisari Justiniani I wa Bizanti ilirudisha utawala wa Kiroma, ila tu katika karne ya 7 uvamizi wa Waarabu Waislamu ulimaliza kipindi cha Kiroma.

Uvamizi wa Waarabu

[hariri | hariri chanzo]

Kuanzia mwaka 642 vikosi vya Waislamu Waarabu kutoka Misri walishambulia eneo la Afrika ya Kaskazini. Mwanzoni hawakufaulu kuwashinda Wabizanti lakini, baada ya uhamisho wa serikali ya makhalifa kutoka Medina kwenda Dameski, Waumawiya walikaza jitihada huko Afrika ya kaskazini.

Mwaka 670 jeshi kubwa la Waarabu likaunda mji wa Kairuan kusini ya Tunis ya leo na mji huu ulikuwa kitovu cha uenezaji. Walipoenea katika Aljeria ya leo walirudishwa na Waberber Wakristo kwa msaada wa Wabizanti lakini jeshi lililofuata lilishinda na kufikia mwaka 711 Afrika ya kaskazini yote (maana yake nchi za leo za Tunisia, Aljeria na Moroko) zilikuwa chini ya utawala wa Waarabu. Hapo sehemu kubwa ya Waberber walifanya haraka kujiunga na Uislamu wakasaidiana na Waarabu.

Matokeo hayo yalikuwa chanzo cha mabadiliko makubwa ya kudumu, maana yake upanuzi wa lugha ya Kiarabu kati ya wananchi na uenezaji wa Uislamu.

Ukoloni wa Wafaransa

[hariri | hariri chanzo]

Historia ya karibuni imeacha kumbukumbu yake inayoonekana katika athira kubwa ya lugha na utamaduni wa Kifaransa kutokana na ukoloni wa Ufaransa kati ya miaka 1830 na 1962.

Kwa Marais wa nchi tangu uhuru, angalia Orodha ya Marais wa Aljeria.

Kwa sasa Aljeria inajenga upya umoja wa kitaifa baada ya vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyoishia mwaka 2002.

Nchi imebaki na idadi kubwa (25-30%) ya wakazi wa kabila la Waberber ambao kihistoria ndio wakazi asilia. Lakini kwa lugha, utamaduni na historia Aljeria ya leo ni sehemu ya dunia ya Kiarabu.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Aljeria kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.