iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.
iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.



Link to original content: http://sw.wikipedia.org/wiki/Gregori_wa_Narek
Gregori wa Narek - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Gregori wa Narek

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Gregori wa Narek alivyochorwa mwaka 1173.

Gregori wa Narek (kwa Kiarmenia Գրիգոր Նարեկացի, Grigor Narekatsi; 951 hivi - 1003 hivi) alikuwa mmonaki na padri wa Armenia maarufu kama mwanafalsafa, mwanateolojia na mtakatifu wa Kanisa la Kitume la Armenia.

Mzaliwa wa familia ya washairi, akiishi katika monasteri ya Narek (Narekavank), ni "mshairi mkuu wa kwanza wa Armenia".[1]

"Kitabu cha Sala", ambacho pengine kinajulikana kama "Kitabu cha Maombolezo", ni kati ya maandishi bora ya fasihi ya Kiarmenia na kimetafsiriwa katika lugha nyingi.

Papa Fransisko alimtangaza mwalimu wa Kanisa tarehe 12 Aprili 2015.

Monasteri ya Narek kabla haijateketezwa.

Gregori alizaliwa Andzevatsik mwaka 950 hivi katika familia ya wakleri wasomi. Baba yake, Khosrov Mkuu, kisha kufiwa mapema mke wake, alipata kuwa askofu mkuu akaandika vitabu muhimu vya teolojia.

Mama alipofariki, Gregori alikabidhiwa alelewe na jamaa yake, Anania wa Narek, mwanzilishi wa monasteri na shule ya kijiji hicho.

Tangu utotoni hadi kifo chake, Gregori aliishi katika monasteri hiyo maarufu kama Narekavank, kwenye Ziwa Van, huko Vaspurakan, Ufalme wa Armenia, leo nchini Uturuki.

Milenia ya kwanza ya Ukristo ilipokaribia kutimia, monasteri ya Narek ilikuwa kitovu maarufu cha elimu kwa Waarmenia. Ikikuwa miaka ya utulivu kabla ya uvamizi wa Waturuki na Wamongolia uliobadili moja kwa moja historia ya Armenia.

Miaka hiyo Armenia ilikuwa inapitia kipindi cha ustawi wa mpya wa fasihi, uchoraji, usanifu majengo na teolojia, ambao ulichangiwa sana na Mt. Gregori, mwalimu wa shule ya monasteri.

Monasteri hiyo ilibomolewa kabisa katika karne ya 20, baada ya Maangamizi ya Waarmenia yaliyofanywa na Waturuki kuanzia mwaka 1915.

Utafiti uliofanywa hivi karibuni kuhusu maandishi yake unadokeza kwamba alifahamu vitabu vya Ugiriki wa kale vilivyotafsiriwa katika Kiarmenia. Kwa mfano, kwamba alijua sana vile vya Plato, Aristotle, Porfiri, Plotino na Filo wa Aleksandria.

Hiyo ilichangia kumfanya ashukiwe kama baba yake kuwa mzushi, yaani kufuata mafundisho ya Mtaguso wa Kalsedonia tofauti na waliofanya Waarmenia wengi.

Kitabu cha Sala

[hariri | hariri chanzo]

Kitabu hicho kimejulikana kwa muda mrefu kama kimojawapo kati ya vile bora vya Ukristo wote.

Gregori alikiita "kamusi elezo ya sala kwa mataifa yote" kwa sababu alitumaini kitaongoza watu wa dunia nzima katika sala.

Akiombwa na wanajumuia wenzake, alilenga kupata jibu kwa swali gumu: "Mtu anaweza kumtolea nini Mungu, muumba wetu, ambaye anavyo tayari vitu vyote na anajua yote vizuri kuliko tunavyoweza kuyaeleza sisi?" Swali hilo walilojiuliza manabii, watunzi wa Zaburi, mitume na watakatifu, alilijibu kwa unyenyekevu – kama mlio wa moyoni.

Katika sala 95, Gregori alitumia uwezo wote wa lugha ya Kiarmenia ili kutafsiri hisia za uchungu na unyenyekevu katika toleo la maneno yaliyofikiriwa kumpendeza Mungu.

Alikiita wasia wake: "herufi zake kama mwili wangu, ujumbe wake kama roho yangu"; ni jengo la imani kwa nyakati zote, la pekee katika fasihi ya Kikristo kutokana na mifano yake yenye ubunifu mwingi, teolojia yake ya dhati, ujuzi wake wa Biblia na unyofu wa mawasiliano yake na Mungu.

Mwaka wa uandishi haujulikani vizuri, lakini ulimalizika miaka 1001-1002, mwaka mmoja kabla hajafa.

Kwake ni lazima lengo kuu la binadamu wote liwe kumfikia Mungu, na kutumia yale yote ambayo umbile linawapatia ili kuungana naye, kwa kufuta tofauti zilizopo kati yao na yeye. Muungano huo unawezekana si kwa njia ya mantiki bali ya hisia. Hapo matatizo ya maisha haya yangekoma.

Maandishi mengine

[hariri | hariri chanzo]

Gregori alifafanua kifumbo Wimbo Ulio Bora (mwaka 977, ambapo alipata upadirisho) na kuandika vitabu vingi vya mashairi, sala na hotuba, mbali ya Historia ya msalaba wa Aparan na kitabu kimoja dhidi ya Watondrakiti (Wapauliciani).

Heshima katika Kanisa Katoliki

[hariri | hariri chanzo]

Gregori ya Narek anaheshimiwa kama mtakatifu na Waorthodoksi wa Mashariki, Kanisa Katoliki la Armenia na Kanisa Katoliki lote, jina lake likiwemo katika orodha rasmi kwenye tarehe 27 Februari[2].

Papa Yohane Paulo II alimtaja katika hotuba mbalimbali[3][4][5] na katika hati Redemptoris Mater[6] na katika barua kwa ajili ya miaka 1,700 ya Ubatizo wa Taifa la Armenia.[7]

Tena anatajwa katika namba 2678 ya Katekisimu ya Kanisa Katoliki.[8]

Tarehe 21 Februari 2015, Papa Fransisko alitangaza nia yake ya kumfanya mwalimu wa Kanisa,[9][10][11] akatekeleza uamuzi huo tarehe 12 Aprili 2015.[12]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Shoemaker, M. Wesley (2013). Russia and The Commonwealth of Independent States 2013. Lanham: Rowman & Littlefield. uk. 211. ISBN 9781475804911.
  2. Martyrologium Romanum
  3. http://w2.vatican.va/content/john-paul-ii/en/audiences/2000/documents/hf_jp-ii_aud_20001018.html
  4. http://w2.vatican.va/content/john-paul-ii/en/angelus/2001/documents/hf_jp-ii_ang_20010218.html
  5. http://w2.vatican.va/content/john-paul-ii/en/audiences/2002/documents/hf_jp-ii_aud_20021113.html
  6. http://w2.vatican.va/content/john-paul-ii/en/encyclicals/documents/hf_jp-ii_enc_25031987_redemptoris-mater.html
  7. http://w2.vatican.va/content/john-paul-ii/en/apost_letters/2001/documents/hf_jp-ii_apl_20010217_battesimo-armenia.html
  8. http://www.vatican.va/archive/ccc_css/archive/catechism/p4s1c2a2.htm
  9. McCarthy, Emer (Februari 23, 2015). "Pope Francis declares Armenian saint Doctor of the Church". Vatican Radio.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. "10th-century Armenian mystic, poet and monk St Gregory of Narek to be a Doctor of the Universal Church", The Catholic Herald, 23 February 2015. Retrieved on 2015-03-11. Archived from the original on 2015-02-23. 
  11. https://www.youtube.com/watch?v=lUFesF-Q880
  12. [1]
  • Grigor Narekatsi. Lamentations of Narek. Mystic Soliloquies with God. Edited and translated by Mischa Kudian. Mashtots Press. London 1977.
  • Grigor Narekatsi. Kniga Skorbi, translated into Russian by Naum Grebnev, Preface by Levon Mkrtchian, Sovetakan Grokh, Yerevan, 1977
  • St. Grigor Narekatsi. Speaking with God from the Depths of the Heart. Translation and introduction by Thomas Samuelian. Yerevan: Vem, 2001.
  • Kéchichian, Isaac, s.j. (introd., trad. et notes). Grégoire de Narek: Le Livre de Prières. Paris: Editions du Cerf, 1961.
  • Mahé, Annie et Jean-Pierre (introd., trad. et notes). Grégoire de Narek: Tragédie, Matean Olbergut'ean, Le Livre de lamentation. Louvain: Peters, 2000 (Corpus Scriptorum Christianorum Orientalium; vol. 584. Subsidia, t. 106).
  • Samwel Poghosyan, "My Narekaci" Yerevan, 2007
  • Grégoire de Narek, Prières, adapté de l'arménien et présenté par Vahé Godel, éd. bilingue, Éditions de la Différence, Orphée, Paris, 1990
  • Luc-André Marcel Garo Poladian, Choix de poèmes arméniens, Hamaskaïne W. Sethian Press, Beyrouth, 1980
  • Luc-André Marcel, Grégoire de Narek et l'ancienne poésie arménienne, éd. Cahiers du Sud, 1954

Muziki uliorekodiwa

[hariri | hariri chanzo]
  • Alfred Schnittke. Choir Concerto (Concerto for Mixed Chorus). Valery Polyansky directs the Russian State Symphonic Cappella. Duration: 45 minutes (43'44"). CHANDOS CHAN 9332 (CD)
  • Alfred Schnittke. Choir Concerto. The Danish National Radio Choir with Stefan Parkman. Chandos Records CHAN 9126. © 1992 Chandos Records (CD)
  • Alfred Schnittke. Compositions for Choir a Capella. Concerto for Choir in 4 Parts, verses by Grigor Narekatsi, Book of Lamentations, or Kniga Skorbi, translated into Russian by Naum Grebnev. Chamber Choir of the Moscow Tchaikovsky Conservatory. Art Director and Conductor Boris Tevlin. Sound director Petr Kondrashin. SFT. © Boris Tevlin 2002. (CD)
  • Collected Songs Where Every Verse is Filled with Grief, arranged by the Kronos Quartet (David Harrington, 1997) from Alfred Schnittke's "Concerto for Mixed Choir." Recorded: 1993-97 Length - 8 min 13 sec Studio / Live: Studio. Performers: Dutt, Hank — Viola ; Harrington, David — Violin; Jeanrenaud, Joan — Cello; Sherba, John — Violin.
  • Nikoghos Tahmizian, Grigor Narekatsi and the Armenian Music from 5th to 15th Centuries (kwa Kiarmenia), 1985, Armenian Academy of Sciences, Yerevan, Armenia.
  • La spiritualità armena. Il libro della lamentazione di Gregorio di Narek, trad. e note di B.L. Zekiyan, Introduz. di B.L. Zekiyan e Cl. Gugerotti, Presentazione di D. Barsotti, Ed.ni Studium, Roma 1999 (kwa Kiitalia)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]