iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.
iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.



Link to original content: http://sw.wikipedia.org/wiki/Eris_(sayari_kibete)
Eris - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Eris

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Eris (sayari kibete))
Picha ya Erisi na mwezi wake

Erisi (alama: ⯰;[1] pia (136199) Erisi au 136199 Erisi) ni sayari kibete kubwa inayojulikana katika mfumo wa Jua letu.

Picha inaonyesha mwendo wa Erisi kwenye picha zilizopigwa kwa darubini ya anga ya Mt. Palomar. Erisi ni ile nukta ndogo inayochezacheza upande wa kushoto juu ya mstari wa katikati ya picha. Mwendo unaoonekana ni mabadiliko ya mahali pa Eris angani katika muda wa masaa matatu. Nukta nyingine ni nyota tu zinazokaa mahali pamoja.

Tabia ze Erisi

Njia yake ya kuzunguka jua ni nje ya njia ya Pluto. Eros inaonekana ina angalau mwezi mmoja unaoitwa Dysnomia. Makadirio ya kipenyo chake ni 2400 km ambacho ni kikubwa kidogo kuliko Pluto. Inazunguka jua katika muda wa miaka 556.7 ya dunia. Umbali wake na jua ni mara 97 umbali wa dunia yetu. Kutoka Erisi hata jua letu laonekana kama nyota ndogo tu.

Kutambuliwa kwa Erisi

Erisi ilitambuliwa 2005 na wanaastronomia walioongozwa na Dr. Michael E. Brown kwenye paoneaanga Mount Palomar (Marekani). Walichungulia picha za anga zilizopigwa mwaka 2003 wakatambua nukta ya anga lililobadilika mahali.

Erisi ni chanzo cha utaratibu wa "Sayari Kibete"

Kutambuliwa kwa Erisi kulisababisha wanafalaki kuanzisha kitengo kipya cha "sayari kibete". Brown aliwahi kutangaza Erisi kuwa sayari ya kumi ya jua letu. Lakini wataalamu wengine waliona uwezekano mkubwa ya kwamba magimba mengine ya kufanana na Erisi yatapatikana karibuni. Maana ya neno "sayari" kwa kulingana na sayari za ndani ilihofiwa kutavurugika. Hivyo utaratibu wa sayari kibete ulianzishwa.

Hivyo Erisi ilikuwa sababu ya kushushwa kwa cheo cha Pluto ambayo ni ndogo kuliko Erisi.


Viungo vya Nje

Habari magazetini

  1. JPL/NASA (2015-04-22). "What is a Dwarf Planet?". Jet Propulsion Laboratory. Iliwekwa mnamo 2022-01-19.