iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.
iBet uBet web content aggregator. Adding the entire web to your favor.



Link to original content: http://sw.wikipedia.org/wiki/Apollo_11
Apollo 11 - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Apollo 11

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
A
Nembo ya Apollo 11

Apollo 11 ilikuwa chombo cha angani cha kwanza kufikisha watu kwenye Mwezi. Hii yote ilifanywa na NASA (Mamlaka ya Marekani ya Usafiri wa Anga). Kilirushwa angani mnamo 16 Julai 1969 kikibeba wanaanga watatu Neil Armstrong, Buzz Aldrin na Michael Collins.

Muundo wa Apollo 11

Chombo chenyewe kilikuwa na sehemu au vitengo tofauti

  • Kitengo cha dambra (command module) penye vifaa vya kuendesha injini, usukani na sehemu walipokaa wanaanga wakati wa safari
  • Kitengo cha huduma (service module) penye injini, matangi ya fueli na oksijeni, vifaa vya mawasiliano
  • Kitengo cha feri ya mwezi yaani chombo cha kufikisha wanaanga wawili kwenye uso wa mwezi na kuwarudisha baadaye kwenye moduli ya jukwaa
Apollo 11.

Sehemu ya jukwaa pekee ilikuwa na oksijeni na shinikizo la hewa kama duniani na hapa wananga waliweza kukaa bila kuvaa suti za anga.

Apollo 11 mwezini

Baada ya kufika kwenye obiti ya kuzunguka mwezi, Amstrong na Aldrin waliingia katika feri iliyotenganishwa sasa na jukwaa na kufika mwezini.

Mnamo 20 Julai 1969 Armstrong na Aldrin walikuwa wanadamu wa kwanza kutua kwenye Mwezi wakati Collins akibaki kwenye obiti karibu na mwezi.

Baada ya masaa 22 feri iliruka tena na kuwarudisha kwenye moduli ya jukwaa. Wanaanga walihamia jukwaa na sehemu ya feri ilibaki katika obiti ya mwezi hadi kuanguka chini baadaye.

Kurudi duniani

Moduli za jukwaa na huduma zilielekea tena duniani. Katika obiti ya dunia moduli zote mbili zilitenganishwa ni jukwaa pekee iliyorudi duniani ikibeba wanaanga na kutua kwa msaada wa parachuti kwenye bahari ya Pasifiki takriban kilomita 24 kutoka manowari iliyowasubiri na kutuma helikopta kuwatoa nje ya maji.

Marejeo