Myanmar
Myanmar (pia: Myama; Myamari) ni nchi ya Asia ya Kusini-Mashariki inayojulikana pia kwa jina la Burma au Bama.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: | |||||
Wimbo wa taifa: Kaba Ma Kyei | |||||
Mji mkuu | Naypyidaw1 | ||||
Mji mkubwa nchini | Yangon | ||||
Lugha rasmi | Kiburma | ||||
Serikali | Win Myint Aung San Suu Kyi | ||||
Uhuru Tarehe |
4 Januari 1948 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
676,578 km² (ya 40) 3.06% | ||||
Idadi ya watu - [[]] kadirio - 2014 sensa - Msongamano wa watu |
(ya 25) 51,486,253 76/km² (ya 125) | ||||
Fedha | Kyat ya Myanmar (K) (mmK )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
MMT (UTC+6:30) {{{time_zone_DST}}} (UTC{{{utc_offset_DST}}}) | ||||
Intaneti TLD | .mm | ||||
Kodi ya simu | +95
- | ||||
1Serikali kadhaa hutambua Yangon kama mji mkuu. |
Imepakana na China upande wa kaskazini, Laos upande wa mashariki, Uthai kusini-mashariki, Bangladesh na Uhindi magharibi.
Kuna pwani kwenye Bahari Hindi yenye urefu wa km 2,000.
Jiografia
haririKaskazini mwa nchi kuna milima mingi. Safu tatu za Rakhine Yoma, Bago Yoma na Nyanda za Juu za Shan zimeanza katika Himalaya na kuelekea kusini. Milima ya Hengduan Shan iko mpakani kwa China. Mlima mkubwa ni Hkakabo Razi kwenye jimbo la Kachin wenye kimo cha mita 5,881.
Mito mitatu mikubwa ya Myanmar inavuka kati ya safu za milima; niː
Mto Ayeyarwady ni mto mkubwa wa Myanmar wenye urefu wa km 2,170. Bonde lake ni la rutuba na lina wakazi wengi.
Karibu nusu ya nchi imefunikwa na misitu.
Miji mikubkwa
haririNafasi mwaka 2006 | Mji | Sensa ya 1983 | Kadirio kwa 2006 | Dola / Mkoa |
---|---|---|---|---|
1. | Yangon (Rangoon) | 2,513,023 | 4,572,948 | Mkoa wa Yangon |
2. | Mandalay | 532,949 | 1,237,028 | Mkoa wa Mandalay |
3. | Naypyidaw (Nay Pyi Taw) * | 0 | 924,608 | Eneo la Kitaifa Naypyidaw |
4. | Mawlamyaing | 219,961 | 451,011 | Dola la Mon |
5. | Bago | 150,528 | 248,899 | Mkoa wa Bago |
6. | Pathein | 144,096 | 241,624 | Mkoa wa Ayeyarwady |
7. | Monywa | 106,843 | 185,783 | Mkoa wa Sagaing |
8. | Meiktila | 96,492 | 181,744 | Mkoa wa Mandalay |
9. | Sittwe | 107,621 | 181,172 | Dola la Rakhine |
10. | Mergui | 88,600 | 177,961 | Mkoa wa Tanintharyi |
11. | Taunggyi | 108,231 | 162,396 | Dola la Shan |
Historia
haririTangu karne ya 9 BK nchi iliona falme mbalimbali zilizotawala kutoka mji mkuu wa Pagan.
Katika karne ya 19 Uingereza ulianza kujishughulisha na habari za Burma (Myanmar) baada ya kutawala maeneo jirani ya Uhindi. Kwa vita tatu kati ya miaka 1826 na 1885 Uingereza ulieneza utawala wake.
Burma ilikuwa sehemu ya Uhindi wa Kiingereza tangu 1885.
Mwaka 1937 Waingereza walianza kutawala Burma kama koloni la pekee.
Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia Japan ilitwaa karibu nchi yote.
Baada ya vita Burma ikapata uhuru wake tarehe 4 Januari 1948.
Serikali iliyochaguliwa kidemokrasia ilipinduliwa na jeshi mwaka 1962.
Mtawala mpya hadi mwaka 1988 alikuwa jenerali Ne Win aliyetangaza siasa ya "Ujamaa wa Kiburma". Upinzani ulikandamizwa vikali mara kadhaa.
Nchi iliona harakati kwa ajili ya demokrasia na dhidi ya udikteta mwaka 1988; hapo Ne Win alijiuzulu.
Baada ya maandamano yaliyokandamizwa mara kadhaa, Jenerali Saw Maung alichukua utawala kwa nguvu ya kijeshi.
Uchaguzi huru wa mwaka 1989 ulileta ushindi wa chama cha NLD, chini ya Aung San Suu Kyi, lakini kamati ya kijeshi ilikataa kukabidhi madaraka.
Burma ilibadilishiwa jina kuitwa "Myanmar" ikaendelea kutawaliwa na serikali ya kijeshi hadi mwaka 2011. Upinzani haukuruhusiwa.
Utawala
haririMyanmar imegawiwa kwa kusudi la utawala katika madola 7 na mikoa 7. "Madola" ni maeneo yanayokaliwa na jumuiya na makabila ambayo ni tofauti na kundi kubwa la taifa linaloitwa Bamar. Maeneo ya Bamar huitwa mikoa.
Madola ya jumuiya ndogo yapo zaidi karibu na mipaka ya nchi. Kuanzia kusini-magharibi ni haya yafuatayo:
- (1) Dola la Rakhaing (Arakan) (Makao makuu: Akjab (Sittwe))
- (2) Dola la Chin (Makao makuu: Hakha)
- (3) Dola la Kachin (Makao makuu: Myitkyina)
- (4) Dola la Shan (Makao makuu: Taunggyi)
- (5) Dola la Kayah (Makao makuu: Loi-kaw)
- (6) Dola la Kayin au Karen (Makao makuu: Pa-an)
- (7) Dola la Mon (Makao makuu: Mawlamyaing)
Halafu kuna mikoa 7:
- (8) Sagaing (Makao makuu: Sagaing)
- (9) Tanintharyi (Tenasserim) (Makao makuu: Tavoy)
- (10) Irawadi (Makao makuu: Pathein)
- (11) Yangon (Makao makuu: Rangun)
- (12) Bago (Pegu) (Makao makuu: Bago)
- (13) Magwe (Makao makuu: Magwe)
- (14) Mandalay (Makao makuu: Mandalay)
Mazingira ya mji mkuu Naypyidaw ni eneo la kitaifa la Naypyidaw.
Madola na mikoa imegawiwa katika wilaya, tarafa, kata na vijiji.
Watu
haririMyanmar ni nchi ya makabila mengi (135 yametambulika rasmi) na lugha nyingi (angalia orodha ya lugha za Myanmar). Kundi kubwa (68%) ni Waburma wenye asili katika milima ya Tibet walikotokea mababu wao miaka 1000 hivi iliyopita.
Lugha kubwa ni Kiburma, ambacho ndicho lugha rasmi.
Wakazi walio wengi (80%) hufuata dini ya Ubuddha, hasa ya madhehebu ya Theravada. Wakristo ni 7%, wafuasi wa dini za jadi ni 6%, Waislamu ni 4%, Wahindu ni 2%.
Picha
haririTazama pia
haririViungo vya nje
hariri- Taarifa za jumla
- General information about Myanmar Archived 16 Oktoba 2015 at the Wayback Machine.
- Burma Myanmar search Engine
- Myanmar Map
- Burma entry at The World Factbook
- Burma Archived 5 Desemba 2009 at the Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs
- Myanmar katika Open Directory Project
- Burma profile from the BBC News
- Myanmar at Encyclopædia Britannica
- Wikimedia Atlas of Myanmar
- Interactive timeline of turning points in Burmese history
- Key Development Forecasts for Myanmar from International Futures
- Online Burma/Myanmar Library: Classified and annotated links to more than 17,000 full-text documents on Burma/Myanmar
- Uchumi
- Taipei American Chamber of Commerce; Topics Magazine, Analysis, November 2012. Myanmar: Southeast Asia's Last Frontier for Investment, By David DuByne
- Kilimo
- Myanmar Business Today; Print Edition, 27 February 2014. A Roadmap to Building Myanmar into the Food Basket of Asia, by David DuByne & Hishamuddin Koh
- Myanmar Business Today; Print Edition, 19 June 2014. Myanmar's Institutional Infrastructure Constraints and How to Fill the Gaps, by David DuByne & Hishamuddin Koh
- Biashara
Nchi na maeneo ya Asia |
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China. |
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Myanmar kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |